Utata dili la Messi kwenda PSG, Perez adaiwa kutia mkono wake ili ampate Mbappe

Suley2019

JF-Expert Member
Oct 7, 2019
1,813
4,545
Punde baada ya Lionel Messi kutangaza kuondoka Barcelona, baadhi ya Wajumbe walianza kujiuzulu nyadhfa zao ndani ya klabu wakilalamika kusalitiwa na Rais Laporta

Wengi wanadai dili la Messi kwenda PSG ni Rais Perez wa Real Madrid anahusika, wakiamini ndie aliemshauri Rais Laporta kwakuwa ni Marafiki huku yeye akiwa na agenda yake

Kwenye barua ya Mjumbe Jaume Lpois aliejiuzulu juzi anasema Perez anamtaka Kylian Mbappe atue Madrid, namna pekee ni Messi kwenda Paris kisha wampate kirahisi kijana wao

Wajumbe wanasema walimchagua Laporta wakiamini atampa challenge sahihi Perez lakini wamezidi kuwa Maswahiba wakubwa na juzi walikuwa wote Camp Nou

Pichani ni Press Release ya Real Madrid kupinga shutma hizo za moja kwa moja kwao

1628682021452.png
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom