h120
JF-Expert Member
- Jan 10, 2012
- 2,530
- 3,315
Kwa wasiofahamu hotel levy ni ushuru wa nyumba za kulala wageni, mlipaji ni mmiliki wa biashara husika, na Ushuru huu unalipwa kwa kufuata Sheria ya nyumba za kulala Wageni(The Hotels Act) ya mwaka 1965 sura ya 105 kifungu cha 26 (2) pamoja na Marekebisho yake ya mwaka 2002 (The Hotel Act Wap. 105) toleo la mwaka 2002.
Kwa utaratibu unaotumika dodoma mjini naona ni mbovu na usio na tija sifahamu kama mikoa mingine wanatumia utaratibu wa aina hiyo, utaratibu uliopo kwa sasa ni wafanyakazi wa manispaa kutembelea kila nyumba ya kulala wageni nyakati za usiku kwa kushtukiza na kukagua kila chumba na idadi ya vyumba vyenye wateja na huzidishwa kwa 1000/=Tshs na kuchukua chao, je hamna utaratibu unaofaa juu ya kusimamia ukusanyaji wa haya mapato kwa njia nzuri zaidi.
Angalizo sipingani na matakwa ya sheria juu ya ukusanyaji wa hotel levy bali njia itumikayo kwa manispaa hiii.
Inawezekana pia utaratibu unaotumika ni sahihi zaidi labda uelewa wangu ni finyu juu ya hili jambo. Naomba tujadili kwa kina je huu utaratibu huu ni sahihi na wenye tija au unapaswa kurekebishwa.
Karibuni.