Utaratibu wa teuzi na ajira serikalini je ipi ni njia sahihi?

conservative3

JF-Expert Member
Nov 12, 2013
1,074
2,000
Samahani naomba isichukuliwe maana tofauti ya kumlenga mtu au kiongozi flani .lengo kujengeana utaratibu bora wa uongozi na madaraka na ni mtazamo tu.

UShauri
Kuanzia waziri, mkuu wa mkoa mpaka mkuu wa wilaya na afisa tarafa ni vema wana siasa na Hata wataalam wakateuliwa. Kuanzia ukatibu mkuu kiongozi,katibu mkuu wizara mbali mbali, Ras, Das, ded iwe wataalam sifa zile za kiutumishi tu. Na utenguzi wao uwe kwa kukosa sifa za kiutumishi na sio za kisasa.

Wajumbe wa bodi angalau isipungue 1/3 wawe wataalam wa hiyo fani.

Nafasi za viti maalumu za ubunge na udiwani wawe watu wenye outstanding performance kwenye Jamii ambapo wanaweza saidia jamii kupita bunge au baraza kufanya maamuzi sahihi.

Hii itatusaidia sana kuwa mfumo mzuri na matokeo ya uhakika kwa wananchi. Utaratibu huo nilio uzungumzia ,je ni vema ukawa wa kimaandishi?

Je, mnaonaje katika hilo?
 

brazaj

JF-Expert Member
Jul 26, 2016
15,189
2,000
Mkuu pamoja na nota bene yako, wale jamaa wa tsis na uvccm bila kuwasahau kina dogo janja na kina nanihii watakuwa wamenuna!
 

Full Blood Picture

JF-Expert Member
Jan 7, 2021
713
1,000
Utaratibu naotumika ni wa katiba ya miaka hiyo. Hivyo mabadiriko yanatakiwa sana kwa sababu unapoingiza wanasiasa kwenye nafasi na mambo ya msingi hapo ndo tunapopiga hatua nyingi kurudi nyuma
 

conservative3

JF-Expert Member
Nov 12, 2013
1,074
2,000
Kuwa na nafasi nyingi za uteuzi zinaimarisha utii wa maelekezo(flow of command) ambapo pia unafifisha/kuzorotesha utaalamu.
unaongea makundi ndani ya jamii kujipendekeza kuchongeana nk.
Faida ya uteuzi kuwa mwingi unaleta mabadiliko (wanaweza kuwa hasi au chanya hapa niyachukulie chanya ikiwa vetting iko sawa sawa).
Faida ya teuzi kuwa nyingi ni alama ya madaraka na mamlaka kwa mteuaji.
Faida ingine ni kujenga mtandao na ulinzi kwa unao waamini.
 

conservative3

JF-Expert Member
Nov 12, 2013
1,074
2,000
Faida za kuwa na TEUZI chache na waajiliwa wengi ni pamoja na
Kukuza muendelezo wa ufanyaji kazi(badala kusubili teuzi/nisubili mkeka)
Matumizi bora ya sheria kanuni na utaratibu wa kazi.
Kupunguza hisia binafsi shida ya kundi au watu wa mtazamo flani.
Kuongea uwajibikaji na idadi na Ufuatiliaji wa utunzaji wa kazi.

Kupunguza risk za serikali kupata hasara kwa maamuzi mabovu,rushwa za madaraka,
Ufuatiliaji na utekelezaji bora wa sera za maendeleo na sera za kimkakati.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom