Utaratibu wa sasa wakupitisha bajeti unalifanya bunge liwe "rubber stamp." | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Utaratibu wa sasa wakupitisha bajeti unalifanya bunge liwe "rubber stamp."

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Byendangwero, May 26, 2011.

 1. B

  Byendangwero JF-Expert Member

  #1
  May 26, 2011
  Joined: Oct 24, 2010
  Messages: 872
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Kulingana na utaratibu wa sasa wa kupitisha bajeti, waziri wa fedha katika hotuba yake ya bajeti uelezea kwa kinagananga jumla yafedha zilizopangwa kutumiwa na serikali kuendesha shughuli zake katika mwaka husika, na chanzo cha fedha hizo. Baada ya kutolewa kwa hotuba hiyo wabunge hupewa wiki nzima ya kuijadili na hatimaye kuipitisha. Baada ya hatua hiyo ndipo bunge uanza kujadili makisio ya wizara moja moja. Kwa mujibu wa maelezo ambayo yamekuwa yakitolewa na spika, bunge likishapitisha hotuba ya bajeti ya waziri wa fedha, biashara inakuwa imeisha; kwakuwa mtu awezi akakubali kitu kizima halafu akakataa sehemu inayounda kitu hicho. Hii ikiwa na maana ya kwamba jumla ya makisio ya wizara moja moja ndiyo yanayounda bajeti inayotolewa na waziri wa fedha, hivyo ikisha pitisha bajeti hiyo ni sawasawa na kupitisha bajeti ya wizara moja moja. Hii ina maana wabunge wetu wanapoteza fedha zetu bure, kutumia mda mwingi kujadili makisio ya wizara wakati tayari walikwisha yapitisha. Ili kujiepusha na jambo hilo ni vema suala la kupitisha bajeti nzima kama inavyotolewa na waziri wa fedha, likahairishwa hadi mwishoni, ili kutoa mwanya kwa wabunge kujua kwanza undani wa bajeti wanayopitisha. Tukubali tusikubali mtindo wa sasa wa kupitisha bajeti ni sawa na kununua mbuzi kwenye gunia.
   
 2. Mtumishi Mkuu

  Mtumishi Mkuu JF-Expert Member

  #2
  May 26, 2011
  Joined: Mar 31, 2011
  Messages: 260
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Mkuu umenena. Ukweli ni kwamba kwa hali halisi ya sasa wanachokifanya wabunge ni kupitisha tu bajeti bila hata kujua kwa kina bajeti wanayopitisha inaenda kufanya nini. Kumbuka pia taarifa za bajeti wabunge hawa wanazipata kwa kuchelewa. Ninakubaliana na wewe kwamba ingetakiwa hotuba ya waziri wa fedha iwe mwishoni kabisa baada ya kuwasilishwa bajeti za sekta moja moja. Hili linawezekana, ni suala tu la kuwaonesha watumishi wetu umuhimu wa jambo hili
   
 3. B

  Byendangwero JF-Expert Member

  #3
  May 26, 2011
  Joined: Oct 24, 2010
  Messages: 872
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Baya zaidi wakati mwingine wanapitisha muswada wa matumizi (appropriation bill) hata kabla ya makisio ya mawizara kujadiliwa. Hali hiyo ndiyo iliyojitokeza katika bajeti iliyopita. Kwakuwa hakuna mantiki yeyote ya kuendelea kupoteza fedha za umma kujadiliana jambo ambalo tayari limekwishapita, safari hii ikiwa bunge litapitisha muswada wa matumizi kabla ya wizara kuwasilisha makisio yao, kuna haja ya wananchi kuandamana nchi nzima, kushinikiza bunge kuhairisha kikao cha bajeti kwakuwa tayari kitakuwa kimepoteza umuimu wake.
   
 4. H

  Hofstede JF-Expert Member

  #4
  May 26, 2011
  Joined: Jul 15, 2007
  Messages: 3,584
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 0
  Nakubaliana na hoja ila unadhani budget inayopitishwa ndiyo itumikayo?. Kinachofanyika bungeni ni mchezo wa kuigiza tu, Kama baada ya budget kupita rais anakuja baadae na kutangaza ongezeko la matumizi kama vile kuongeza mishahara ni dhahiri bunge litaendelea kuwa rubber stamp as long as CCM wanauwezo wa kuchakachua matokeo ya kura kujipatia quoram ya wabunge wa kupitisha mambo yao. Tukiwa na bunge na wabunge wengi wa upinzani wenye uwezo wa kuzuia maamuzi yasipite hapo ndipo tutakapopata bunge huru.
   
 5. Chapakazi

  Chapakazi JF-Expert Member

  #5
  May 26, 2011
  Joined: Apr 19, 2009
  Messages: 2,881
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  mhh...interesting! Kama madai yako yana ukweli, basi hii ni ishu kubwa sana! Inaelekea hatujui maana ya Bajeti Tanzania! Huwezi kupitisha bajeti bila kusikia break-down yake. Huu ni WIZI!
  Unakumbuka ishu ile ya december ya kuwa na bajeti mbili? Ule nao ni WIZI. Katika nchi nyingine yeyote serikali lazima ianguke.
   
 6. Chapakazi

  Chapakazi JF-Expert Member

  #6
  May 27, 2011
  Joined: Apr 19, 2009
  Messages: 2,881
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Nimeipenda hii topic sana kwa sababu ya interest yangu in public finance na sheria.
  Katika kufanya research kidogo, nimekutana na hii: http://www.parliament.go.tz/bunge/Docs/books/bungemuundo.pdf
  Ni kitabu kimeandikwa na Pius Msekwa juu ya Bunge la Tanzania, Muundo wake, Majukumu yake, na utekelezaji wa majukumu hayo.
  Sehemu ya IV (p20) inazungumzia juu ya upitishaji wa bajeti. Mh Pius anatoa maelezo mazuri lakini bado hayajibu kiini cha swali. Anaongelea kutopitishwa kwa bajeti nzima lakini sio kwa bajeti za wizara mbalimbali.
   
Loading...