Utaratibu wa Rais kuongea na Taifa kila mwisho wa mwezi uliishia wapi?

Ntozi

JF-Expert Member
Feb 1, 2021
226
299
Huu utaratibu ulikuwa unaleta shauku Kwa wananchi na majibu mengine yalipatikana kupitia utaratibu huu.

Kuna wakati wananchi wanakuwa na shauku ya kujua kinachondelea nchini juu ya mambo mbalimbali yanayokuwa yanaendelea.Na wanakuwa na imani kuwa mwenye majibu ya mwisho ni Rais wa nchi.

Ni wachache wenye uelewa wa kweli juu ya kupanda bei vifaa vya ujenzi, petrol,mbolea kwa wakulima na bidhaa zingine.wanahitaji kauli ya Rais badala ya ramli chonganishi kwenye mitandao ya kijamii. ule utaratibu ulikuwa na ubaya gani?Au ndiyo kila Zama na kitabu chake basi?
 
Tuache utani,
Kuna issue za taasisi ya urais zilikuwa zina unguruma enzi za NKAPA.
Siku ikitolewa taarifa Rais ataongea na Taifa hakika kulikuwa na msisimko fulani
 
Huu utaratibu ulikuwa unaleta shauku Kwa wananchi na majibu mengine yalipatikana kupitia utaratibu huu.
Kuna wakati wananchi wanakuwa na shauku ya kujua kinachondelea nchini juu ya mambo mbalimbali yanayokuwa yanaendelea.Na wanakuwa na imani kuwa mwenye majibu ya mwisho ni Rais wa nchi.
Ni wachache wenye uelewa wa kweli juu ya kupanda bei vifaa vya ujenzi, petrol,mbolea kwa wakulima na bidhaa zingine.wanahitaji kauli ya Rais badala ya ramli chonganishi kwenye mitandao ya kijamii. ule utaratibu ulikuwa na ubaya gani?Au ndiyo kila Zama na kitabu chake basi?

Sent from my Nokia 5.1 Plus using JamiiForums mobile app
Kila zama na mambo yake, mtoa hutuba alijauz mashirikacyote ya ummz kwa sholingi mbili. Kuna Rais alikuwa anawaita Ikulu kina tundulissu kula daku kila wakilialia kutikisa kiberiti, hadi Mnyika akasema Kikwete ni dhaifu.
 
Huu utamaduni wa kuhutubia taifa kila baada ya muda fulani ulianzia kwa Nyerere, haukuwa rasmi kila mwezi bali ulikuwa kila mara ndani ya mwezi. Mkapa akaufufua na kuuweka kuwa rasmi kila mwezi, na Mkapa aliupenda sana (maana ilifika wakati alikuwa hoi hospitalini akifanyiwa operation ya nyonga huko Uswisi na kutokea huko huko Mkapa akahutubia taifa!).

Mwanzoni mwa utawala wa Mkapa huo utaratibu ulivutia watu lakini baadaye ukawa ni uchafu mtupu, ukawa unabowa na kuchosha watu, maana hotuba hazikuwa na jipya

Kikwete alipoingia madarakani akaamua kuuiga, bahati mbaya ukamtokea puani (sakata la Dowans/Richmond likamfanya auche, maana ulimvua nguo), mwisho wa siku akauua kimya kimya.

Alipokuja Magufuli yeye akaibuka na utaratibu wa kutembea kabisa na media zote, popote atakapokuwapo ataruka live na hiyo itachukuliwa ni hotuba ya rais kwa taifa. Magufuli hata akiwa kanisani akishukuru kupewa ekaristi, basi nayo itaruka kama hotuba kwa taifa!

Yote kwa yote ni utaratibu wa kipropaganda hauna chochote cha maana kwa mtanzania. Samia hauwezi (hana fikra za kuweza kuongea mara kwa mara kwa taifa) na akijaribu utamtokea puani.
 
Amekwisha poteza mvuto kwa kutaka kila siku aonekane mbele ya kamera nafikiri watu awavutiwi na hotuba zake kwa mwanzo ilivyokua.

Kama akiamua kurejesha huo utaratibu aweke na uhuru wa waandishii kuuliza maswali baada ya hotuba.
 
Jiwe alikuwa anaboa Watz wengi (Wenye akili lakini)
 
Huo utaratibu wa kuongea na taifa kila mwezi ilikuwa ni propaganda tu zenye lengo LA kufukia mashimo kwa serikali juu ya jambo lolote lilikuwa linaonekana linaitia doa serikali.

Che Nkapa alikuwa yuko vizuri katika hilo iwe ni juu masuala ya wapinzani wake kisiasa,kichama,kiserikali,kijamii na nk.

Alikuwa akigusia mambo mbalimbali lakini katika hayo kuna lile haswaa kusudiwa,na alifanikiwa sababu alikuwa ni intellectual mzuri tu.

Sasa zama zimebadilika badala ya kuhutubia taifa Rais anakuwa na "Chawa" wakumsemea badala yake. Utasikia" Mwenyekiti wa UVCCM amekemea na kulaani vikali juu ya mwenendo wa Humphrey SlowSlow na Gwajiboy kutoa kauli za kuwachanganya wananchi kuhusu suala zima LA chanjo".

So kwa mfano huo utaona kuwa zama zimebadilka mgawanyo wa mamlaka umesogezwa kwa vijana ktk suala zima LA wakosoaji na wapinzani wa taasisi ya urais.baada ya muda utaskia amechaguliwa kuwa mkuu wa wilaya kinondoni baadae tunapata kina Bashite.

Nadhani umenipata kidogo
 
Huu utaratibu ulikuwa unaleta shauku Kwa wananchi na majibu mengine yalipatikana kupitia utaratibu huu.
Kuna wakati wananchi wanakuwa na shauku ya kujua kinachondelea nchini juu ya mambo mbalimbali yanayokuwa yanaendelea.Na wanakuwa na imani kuwa mwenye majibu ya mwisho ni Rais wa nchi.
Ni wachache wenye uelewa wa kweli juu ya kupanda bei vifaa vya ujenzi, petrol,mbolea kwa wakulima na bidhaa zingine.wanahitaji kauli ya Rais badala ya ramli chonganishi kwenye mitandao ya kijamii. ule utaratibu ulikuwa na ubaya gani?Au ndiyo kila Zama na kitabu chake basi?

Sent from my Nokia 5.1 Plus using JamiiForums mobile app
Ni wakati wa mkapa
 
Mbona anaingea kupitia G.Msigwa kila wiki

Back
Top Bottom