oba
JF-Expert Member
- Oct 31, 2010
- 309
- 65
Utaratibu uliotolewa na bodi ya mikopo mwaka huu umehisiwa kuleta mifarakano katika familia baada ya familia kadhaa kushangilia baada ya kuona watoto wao wamepata mfano 2,500,000 ambayo kwao inaonekana ni kubwa kwani hawajawahi kushika hata 1,000,000. Wazazi wanashangilia kuwa pesa hizo zitawasaidia na wao pia huku wakiwa hawafahamu gharama ya masomo chuoni na kuwa wanatakiwa waongezee pesa ili kuchangia gharama za masomo hayo.
Kwa sababu hiyo watoto watachukiwa na wazazi eti kwa kujipenda na kumaliza mamilioni ya pesa peke yao na watoto watawachukia wazazi kwa kushindwa kuwaongezea pesa zilizopungua kwenye gharama za masomo.
Nawasilisha!