Murashani GALACTICO
JF-Expert Member
- Feb 27, 2012
- 2,205
- 4,707
Wanajukwaa la elimu. Mm ni mtumishi mwalimu katika shule ya sekondari hapa Tanzania. Naomba kufahamu namna manumuzi ya vifaa vya kujifunza na kufundishia ulivyo kwa shule za serikali. Kwa uelewa wangu mdogo wa sheria ya manunuzi ya umma PPRA na marekebisho yake ya 2016 napata wakati mgumu na kujikuta sielewi jinsi inavyopaswa vifaa na hudumu ,kandarasi na zabuni kwa shule. Mathalan najua bei za katoni ya chaki, katon za ream A4 na A3 bei za vifaa vya maabara na vifaa vingine vingi vitumikavyo mashuleni. Sasa kila nikijaribu kushauri wakubwa wangu wa kazi hapa kituo nilichopo wananiona mtu tofauti sana. Kwan vitu, huduma na vifaa hununnuliwa kwa mtindo wa cheki na zabuni kwa gharama za juu kuliko kawaida yani. Naomba tujikite kwenye hoja na sio vioja kwa maslahi ya umma