Wakati UDART wameonesha waziwazi kufeli juu ya matumizi ya CARD kwa maksudi!
TEMESA nao pasipo kujua ama kwa maslahi yao binafsi, Wameingia kichwa kichwa katika matumizi ya malipo ya N-CARD bila weledi!
Abiria wote wameelekezwa kuhakikisha wanatumia N-CARD ili kuweza kulipia kivuko, Hivyo wametangaziwa Ukomo wa matumizi ya tiketi za kawaida ifikapo tarehe15/5
Jambo ambalo limechangia idadi kubwa ya abiria kununua na kusajili CARD kiasi cha kuibua kero kubwa zifuatazo;
Waziri fuatilia haraka utendaji wa N-CARD (Busy hour) TEMESA ili baadae USISIKITIKE Kama maamuzi ya TFF

- Mashine za kuscan Card Zipo mbili tu kwa kila upande, na mda wa kusubiria kuscan kwa kila mtu mmoja ni sekunde 3-4 ( Delay Scan Cycle time), Hivyo kwa uwezo wa kivuko cha MV magononi watu 2000, Maana yake watu hao wataingia kwenye kivuko kwa sekunde 8000sec ukiachilia zile za magari na mikokoteni! Mda huo ni sawa na dakika 134, kwa mashine mbili maana yake watavuka kwa dakika 67 sawa na lisaa limoja na dakika 7! Kwa maana hiyo abiria watatumia mda mwingi ili kuvuka kuliko mtu anaesafiri na Boti kutoka Dar kwenda Zanzibar! Ni ujinga mkubwa sana
- Namna ya kuongeza na kuangalia salio kwenye N-CARD ni lazima mtu awatafte wao wenyewe, Huwezi kurecharge kwa mitandao ya simu.
- Kiwango cha kurecharge CARD lazima kianzie 1000, jambo ambalo linawatenga wale wasiyo na elfu moja zaidi ya kupewa Mia mbili ya kuvukia kila siku! (kama mia mbili iliwapa tabu hiyo elfu moja wataipata wapi? Kwanini kiwango kisingekuwa kuanzia 200?).
- Mfumo huo wa N-CARD umekuwa ukifyeka pesa za abiria bila taarifa inapotokea hitilafu za kiufundi ( January mfumo huo ulikomba pesa zote kwenye N -Card za wateja pasipo taarifa na kila aliyelalamika walimuahidi kumrejeshea pasipo kufanya hivyo.
- Ulazima wa N-CARD unamlazimisha hata anaevuka kwa siku moja awe na Kadi kwa mujibu wa maelezo kwenye tangazo lao
Waziri fuatilia haraka utendaji wa N-CARD (Busy hour) TEMESA ili baadae USISIKITIKE Kama maamuzi ya TFF