Utaratibu wa magari ya Rombo kuondoka yote saa 12 kamili ni wa kishamba sana

themagnificient

JF-Expert Member
Dec 13, 2016
988
3,318
Sijawahi ona sehemu yenye usafiri ambao gari zote zinaondoka wakati mmoja mapema sana kama Rombo, Tarakea

Yani gari zote zinaondoka saa 11 hadi 12 kamili yaani huwezi kuta basi ya saa 1 au saa mbili hadi saa nne hivi huwa mnakimbiliaga wapi warombo?

Amgalieni mtwara gari hadi zaa saa sita sio kila mtu anataka kukimbizana asubuhi asubuhi
 
Sijawahi ona sehem yenye usafiri ambao gari zote zinaondoka wakati mmoja kama rombo, tarakea

Yani gari zote zinaondoka saa 11 hadi 12 kamili yaani huwezi kuta basi ya saa 1 au saa mbili hivi huwa mnakimbiliaga wapi warombo?
Ukiona zinawahi nakushauri kazisubiri Marangu Mtoni, hapo zinachelewa kuondoka.
 
Sijaelewa Yaani LATRA Labda Huko Wafanyabiashara Waombe Ratiba Ya Saa Moja
 
Sijawahi ona sehem yenye usafiri ambao gari zote zinaondoka wakati mmoja kama rombo, tarakea

Yani gari zote zinaondoka saa 11 hadi 12 kamili yaani huwezi kuta basi ya saa 1 au saa mbili hivi huwa mnakimbiliaga wapi warombo?
Halafu wanavyokimbizana sasa...
Yaani mpaka wavuke njia panda ya Himo ndio waananza kutuliza wenge.
Kuna siku walitaka kuniacha pale Kiboro huku nikiwa tayari nimeshakata tiketi kwa ajili ya ligi tu na hiyo ni 12 kasoro robo asubuhi!.
 
Sijaelewa Yaani LATRA Labda Huko Wafanyabiashara Waombe Ratiba Ya Saa Moja
Mleta mada anajichanganya, anasema yanaondoka kati ya saa 11:00 na 12:00 asubuhi haoni kuna la 11:00, 11:15, 11:30, 11:45 na 12:00 asubuhi, angeshauri muda wa kupishana badala ya kulalama na kuwaita wenye mabasi washamba!
 
Halafu karibu tu inashangaza sana ilitakiwa ziwepo had bus za saa 4 kama mtwara... Mana huko na mtwara umbali unakaribiana...
 
Nafikiri mleta mada unakosea mahali pamoja, Rombo ni wilaya sio makao makuu ya mkoa. Nitaje wilaya moja ambayo sio makao makuu ya mkoa ambapo gari za mkoani zinaanzia na kusafiri muda huo unaotaka Wewe.
Gari inayotoka Rombo inawahi kujazia abiria njiani na stand kuu Moshi
Ukitaka kusafiri muda huo nenda stand kuu ambayo ni Moshi mjini hata mchana unapata chuma ya Dar nk
 
Kyela ,mbinga , mpanda ,kahama ,musoma hizo sehemu zote sio makao makuu ya mkoa na basi zinaanza safari saa 12
Ama labda sijakuelewa
 
Sijawahi ona sehemu yenye usafiri ambao gari zote zinaondoka wakati mmoja kama Rombo, Tarakea

Yani gari zote zinaondoka saa 11 hadi 12 kamili yaani huwezi kuta basi ya saa 1 au saa mbili hivi huwa mnakimbiliaga wapi warombo?
Mjinga sana wewe, watu wanawahi shughuli mapema wewe unataka udebwedo.
Zwazwa haswaaa wewe
 
Nafikiri mleta mada unakosea mahali pamoja, Rombo ni wilaya sio makao makuu ya mkoa. Nitaje wilaya moja ambayo sio makao makuu ya mkoa ambapo gari za mkoani zinaanzia na kusafiri muda huo unaotaka Wewe.
Gari inayotoka Rombo inawahi kujazia abiria njiani na stand kuu Moshi
Ukitaka kusafiri muda huo nenda stand kuu ambayo ni Moshi mjini hata mchana unapata chuma ya Dar nk
Pale unapokospa kumbe hata wewe hujui.

1. Kilwa Masoko kuna basi hadi za saa tisa kwenda Dar

2. Mugumu serengeti kuna nasi za saa nne kwenda Mwanza

3. Kibaya (Kiteto kuna basi za saa nne kwenda Dar

Niendelee?

Je hiyo miji niliyoitaja ni makao majuu ya mikoa yao?

Nadhani kitemdo cha kuwa na mda tofauti wa mabasi kuondoka inategemea na idadi ya abiria labda pia uamuzi wa wamiliki

Sent from my TECNO CD7 using JamiiForums mobile app
 
Halafu wanavyokimbizana sasa...
Yaani mpaka wavuke njia panda ya Himo ndio waananza kutuliza wenge.
Kuna siku walitaka kuniacha pale Kiboro huku nikiwa tayari nimeshakata tiketi kwa ajili ya ligi tu na hiyo ni 12 kasoro robo asubuhi!.
Sijui wanawahigi wapi wasije wakaja kubwaga watu.kwenye zle kona
 
Back
Top Bottom