Utaratibu wa mabasi ya Abood kuingia gereji Morogoro una faida gani?

MZEE CHAKA

Member
May 27, 2021
87
141
Mabasi ya kampuni ya Abood yanayotokea popote, yakifika Morogoro, lazima yapitie kwenye yard yao. Abiria wote mnashushwa nje ya geti. Basi linaingia ndani, sijui linaenda kufanyiwa nini? Halafu baada ya dakika kadhaa linatoka. Abiria mnapanda tena kuendelea na safari.

Hapo nje hakuna sehemu rasmi ya kusubiria. Mnatelekezwa juani, eneo la wazi, mnalowana vumbi. Sijui kama suala hili lipo kisheria? Serikali ya mkoa, waziri wa usafirishaji na uchukuzi. Waziri wa mambo ya ndani, waziri mkuu na hata rais wetu, sijui kama wanalifahamu hili?

Mimi kwa upande sikupendezwa na kilichotokea leo tarehe 23-10-2021. Kwangu ni mara ya kwanza, lakini nilivyosikia toka kwa abiria wenzangu tuliyotokea Mbeya, kwa basi la Abood lenye namba T830AWY, kwamba huu ndiyo utaratibu wao. Lazima mabasi yao yote yapitie ofisini kwao. Abiria wote tulishushwa, gari likaingia ndani ya ofisi zao, halaf likatoka tukaendelea na safari ya Dar. Sidhani kama na mabasi mengine yanafanya hivi? Ingawa juzi nilipanda basi la Majinja sijaona mambo hayo
 
Huo sio tu utaratbu, ni sharti. Hata abood mwenyew hana namma sijui umenierewa??
 
Nilipanda Kandahar kwenda Moshi tulipofika Arusha tulishushwa pia gari ikaingia nadhani kujaza mafuta na mambo mengine.
 
Back
Top Bottom