Utaratibu wa Kuwaondoa Majaji Vibaraka

Hamatan

JF-Expert Member
Nov 10, 2020
3,182
7,642
Mheshimiwa sana Tundu Lisu aliwahi kutamka Bungeni kuwa mahakama ilikuwa imenijisiwa kiasi cha kuwa na majaji ambao hawana hata uwezo wa kuandika hukumu. Swali la kujiuliza, je Rais kwa nini awateua majaji ambao hawana uwezo?

Kule Mbeya, CHADEMA waliwahi kueleza kuwa hukumu ya Sugu iliandikwa ofisini kwa mkuu wa mkoa, na kwamba hukumu ile ilikiwa ya uonevu. Madai haya yalipata nguvu kutokana na rufaa ya Sugu ambapo mahakama kuu ilikubali rufaa ya Sugu, na kutamka wazi kuwa hakuwa na kosa.aana yale ni kuwa hakimu yule au alikuwa kibaraka au alikuwa na uwezo mdogo wa kutafsiri sheria.

Jambo la ajabu ni kuwa yule hakimu aliyemwonea Sugu, Rais alimzawadia ujaji. Yaani hakimu ambaye au alitenda dhuluma au ana uwezo mdogo, akapewa ujaji. Je, majaji wa namna hii tunao wangapi? Na hawa majaji wa kipindi kile cha giza totoro, tunaweza kuwaondoa kwa namna gani ili kuipa mahakama heshima inayostahili?

Unajisi mkubwa uliofanywa na awamu ya 5 ni kuingiza TISS mahakamani.

Mahakama haitakuja kuwa huru mpaka wale majaji/Mahakimu TISS waondolewe kwenye mahakama. La sivyo, ukweli hatuna mahakama.
 
Mahakama zetu ni UOZO MTUPU! Sasa zinatumika kuminya haki ya Watanzania wengi sana. Mahakama ni adui mwingine mkubwa wa Watanzania baada ya maccm, polisiccm ya tatu ni mahakama.
 
4 Reactions
Reply
Back
Top Bottom