Utaratibu wa kutumia kadi kwenye mabasi ya mwendokasi kuanza kesho

Kurzweil

JF-Expert Member
May 25, 2011
6,622
8,410
MRADI wa Mabasi Yaendayo Kasi jijini Dar es Salaam (UDART) umeanzisha huduma kwa wateja wao za kutumia kadi maalumu wakati wa kupanda mabasi hayo itakayoanza rasmi kesho.

Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam leo asubuhi, Mkurugenzi Mtendaji wa UDART, David Mgwasa alisema wameanza kutoa huduma hiyo ya kadi ili kuwarahisishia wateja wao na kuondoa changamoto ya kusubiri tiketi kwa muda mrefu kabla ya kuondoka.

Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya MaxMalipo ambao wameingia ubia na Udart katika matumizi ya kadi hizo, Mhandisi Juma Rajabu alisema kwamba kwa kuanzia wametoa kadi 200,000 ambapo kila kadi itauzwa kwa shilingi 5000 ingawa bei halisi kwa kadi moja ni shilingi 500 na sh.4500 inayobaki itakuwa ni malipo ya mteja wao.

“Shilingi 4500 zitatumika kama malipo ya nauli kwa siku saba hadi nane kwa kwenda eneo lolote na kuwa kadi hizo zitapatikana katika vituo vya Kimara, Mbezi, Morocco, Gerezani, Posta na kuwa zitakuwa ni endelevu” alisema Rajabu

Chanzo: CloudsFm
 
Najuta kupanda hayo mabasi jana nilitoka Kisutu saa nne nikiwa nataka nielekee Msimbazi... nilikaa kituoni kana Dakika tano likaja basi likaelekea fire nikashuka niunganishe kuelekea msimbazi... pale nilikaa zaidi ya dakika arobaini nilijuta abiria wenzangu walipoona miyayusho wakawa wanadai malipo yao wakaondoka nikabaki mie mkuda maana ndio siku yangu ya kwanza nikavumilia niliomba na mimi kurejeshewa nauli wakaniambia wewe haiwezekani sababu umetokea kisutu ila nikawaambia ndio nikeshe huku kituoni ambapo hamna hata siti za kukaa lol... basi likaja bus likabeba wate wabishi likasema linaenda na feri likitokea gerezani. Bus likasimama msimbazi nikaona kituo cha kwanza hakinifai kuna kituo cha pili sikushuka cha kwanza basi likafika kituo cha pili likasepa bila kusimama lol nikasema lol sina ujanja ila gerezanisishuki... nikageuza nalo hadi kile kituo cha gerezani nusura dereva apitilize ila akaambiwa apakie abiria nadhani akili yake ni kupeleka watu feri nikajishukia na mpira kipindi cha kwanza chote nilikosa kukitizama...

Nimegundua haya mabus si ya mwendo kasi madereva wana akili za kama za madereva wa dala dala tu.... makutano ya barabara ya msimbazi na Uhuru kuna wachina na gari lao la namba za ubarozi lilijiingiza robo kwenye barabara ya mwendo kazi bahati yao dereva wetu alimstahi akampigia honi and then wachina fasta wakarejesha gari lao na nimegundua Madereva wa Mwendo kasi hawafuati Taa za Usalama maana karibu njia nzima alikuwa anapita on red right. Bus Lefu kama icarus linaendeshwa ovyo ovyo...
 
Kwa wakazi wa Dar wengi ni bora wakawa na kadi mtindo wa kupanga foleni unapoteza sana muda.Kadi ni mzuka sana.Ila UDA RT wajue kusoma flow ya abiria kama siku ya leo Kariakoo kulikuwa na Abiria wengi sana mchana lakn nasha gaa wao UDART wameyapark tu mabasi pale Jangwani
 
Km cku nyngne cpand inakua vp wanakata hvy hvy cku saba??
4500 haitumiki kwa siku saba inatumika kwa Trip sits.Kila route moja wanachaji 650 kwa hiyo kwa trip sita inakuwa 3900 kwenye 4500 inabakia 600,Hapo unaongeza tu Salio unaendelea kutumia.Sio lazima usafiri siku zote ndani ya siku saba.
 
Back
Top Bottom