Utaratibu wa kutumia Detention Register ya Polisi ukoje? Ni kila mwaka na Register mpya au ni mpaka iliopo ijae?

Salary Slip

JF-Expert Member
Apr 3, 2012
47,013
144,371
Hili jambo kuna watu wanalielewa vizuri sana na wanaweza kusaidia jamii kujua ukweli ila Watanzania tumekuwa waoga na hivyo wenye kujua wamechagua kukaa kimya.

Upotoshaji unapata nafasi kwasababu hii kesi ni ya kisiasa kiasi kwamba hata Polisi wanaolewa utaratibu ukoje wanaweza wasiseme ukweli. Kwahiyo inahitajika watu wenye kuaminika na wasio na upande wajitokeze na kusema ukweli hadharani.

Huyu hapa ni wakili maarufu anaejulikana kama Baba Mwita katika mtandao wa twitter akionyesha kushangazwa na jinsi hii Detention Register ilivyorekodiwa katika kesi ya Mbowe.

All in all, kama Detention Rigester ni hiyo hiyo moja kama inavyodaiwa na huyu Wakili hapa chini,, basi hiki ni kituko cha mwaka.

Msome hapa:

Dentition Register (D.R) Inaonyesha Mtu Wa 392 Kuingia Mahabusu Central ni Lingwenya Tarehe 12/8/2020 Cha Ajabu Ni Kwamba D.R Hiyohiyo Inaonyesha Mtu Wa 114 Aliingia 30/7/2021 Na Mtu Wa 156 Aliingia 3/8/2021 N.k Yaani Mtu Wa 114 Aingie 2021 Yeye Wa 392 Aingie 2020? D.R Hiyohiyo?

Haya hapa chini nayo ni maelezo ya Shahidi mahakamani kama yalivyotolewa kupitia twitter na Martin Maranja Masese, maelezo yanayoongeza utata wa hili jambo.

Maelezo ya Shahidi wa Jamuhuri Mahakamani:

Shahidi wa Jamhuri jana, Afande Msemwa anasema Detention Register ambayo ina majina ya Adamoo na Ling'wenya ilianza kutumika 14 July 2020 na kufungwa 12 August 2020 lakini ndani yake kuna tarehe za 2021 kasoro ukurasa wa akina Lingwenya na Adamoo. Mambo ya hovyo sana yanafanyika!
 
Tusome hapa: Dentition Register (D.R) Inaonyesha Mtu Wa 392 Kuingia Mahabusu Central Ni Lingwenya Tarehe 12/8/2020 Cha Ajabu Ni Kwamba D.R Hiyohiyo Inaonyesha Mtu Wa 114 Aliingia 30/7/2021 Na Mtu Wa 156 Aliingia 3/8/2021 N.k Yaani Mtu Wa 114 Aingie 2021 Yeye Wa 392 Aingie 2020? D.R Hiyohiyo?
Halafu bado kuna mtu anakuja kufananisha ushahidi huu na ushahidi wa kesi ya DC wa mwendazake.
 
Yote hayo ni 9. La 10 ni je, adamoo ypo au hayupo, ni mtu kiwiliwili au ni jini lisiloonekana? Si yupo?
 
Sasa hivi majaji wanadanganywa kama vilaza kesi hiyo bora ingesikilizwa hata mtendaji wa kijiji angehoji uhalali wa hiyo D.R kuliko hawa majaji uchwara
Teuzi zinazozingatia uovu zilizo asisiwa na Jiwe na kurithiwa na Saa 💯 zimewageuza Wasomi wa Tanzania kuwa Mahayawani kabisaa.
 
Back
Top Bottom