UTARATIBU wa Kura ya Maoni Uboreshwe.....!

TUJITEGEMEE

JF-Expert Member
Nov 6, 2010
23,909
23,072
Jana nilibahatika kuanagalia Bunge kwa muda mchache kabla vipaza sauti hivijapata hitilafu. Bahati mbaya sijapa muswada washeria inayotungwa kuhusu suala la upitishaji wa katiba mpya ambao hasa ndiyo uliokuwa ukijadiliwa hiyo jana jioni. Kikubwa nilichoelewa ni kuwa itapigwa kura ya maoni, ambayo mpigaji kura hiyo atachagua ndiyo au hapana kukubali au kukataa Katiba mpya iliyotungwa. Ilielezwa kuwa kura hii ilitumika huko Zanzibar kuipata serikali ya umoja wa kitaifa(nadhani walitakiwa waseme serikali ya umoja wa wazanzibar- hili linahitaji mjadala mwingine).

Binafsi ninadhani kura hii isitumike kama ilivyotumika huko Zanzibar. Kwa sababu kufanya hivyo hakutoi huru kwa mpiga kura kuchagua hasa katiba halisi anayoitaka. Mfano, kwenye katiba kunaweza kuwemo na vipengele kama vitatu kati ya ishirini vya katiba yote, ambavyo mpiga kura anaona vipengere hivi vikiachwa vitaleta madhara makubwa kwenye uongozi wa serikali yetu tunayoitaka kutokana na Katiba hii mpya; lakini vipengele vingine kumi na saba vikawa ni vizuri sana kwa mustakabali wa nchi yetu. Sasa kutokana na unyeti wa vipengere hivi vitatu, huyu mheshimiwa ataamua kupiga kura ya hapana. Kwa kweli hapa mpiga kura atakuwa amenyimwa uhuru wa kuchagua vile vipengere 17 ambavyo aliona viko safi kabisa. Mtindo huu ukiendelea kwa wapiga kura wote tunaweza kukataa katiba ambayo ilikuwa na makosa machache. Na hili litaliingizia taifa hasara kubwa kutokana na gharama ambayo imetumika kuendesha mchakato huu. Vinginevyo ielezwe kabisa kuwa kama katiba ikikataliwa basi wajumbe wote na wabunge wa bunge la katiba waliohusika warudie kazi hii bila malipo (ukizingatia wamepewa pesa nyingi za watanzania kuendasha mchakato huu).

Sasa ili kuepuka hili kura ya maoni ipigwe kwa kufuata vifungu vya katiba. Vifungu hivi vigawanye katika makundi matatu. Kila kundi la vifungu vya katiba mpya lipigiwe kura ya ndiyo na hapana. Kikundi au makundi ya vifungu hivi kitakacho/vitavyokataliwa (kwa kupata kura chache) yarudishwe kwenye bunge la katiba ili yaboreshwe, na kura irudiwe kupigwa ili wananchi wajiridhishe kuwa vifungu viko sawa.

Utaratibu huu wala hautawasumbua wapiga kura kwani walishazoea kupiga kura ya rais, mbunge, na diwani (makundi matatu) kwa wakati mmoja. Kwa kweli utaratibu huu ukikubaliwa utatoa huru mkubwa kwa mpigakura katika kuikubali au kuikataa katiba mpya anayoitaka, na tutapata Katiba mpya Kweli tunayoitaka.

Haya ndiyo maoni yangu.

Nakaribisha maoni yako pia kuhusu upigaji kura ya maoni kuchagua kukubali ama kuikataa Katiba mpya.


-MpigaKelele.
 
Back
Top Bottom