Utaratibu na gharama za kupima vinasaba (DNA) Tanzania

Mkuu Baba Ubaya,mashauri yote juu ya watoto yanasimamiwa na Sheria ya Mtoto,2009 pamoja na Kanuni zilizotengenezwa kwayo.Yeyote anayetaka kushughulika na suala la mtoto afungue shauri kulingana na Sheria tajwa.

Fahamu ya kuwa,mtoto ni yule mwenye miaka chini ya kumi na nane(18). Amri ya kupima DNA hutolewa na Mahakama tu pale itakapoona kuna haja ya kufanya hivyo. Suala la mtoto ni suala nyeti na ni lazima limalizwe na Mahakamani kwa mujibu wa sheria.
 
Last edited by a moderator:
Mkuu kwa utaratibu wa kupima DNA watusaidie wanaoelewa zaidi, mimi napenda kuchangia kwenye upande hasa wa kijamii, kama mtoto kwa sasa ana miaka 18, na anamfahamu baba mmoja toka akiwa mtoto, nasasa kapatikana mwingine, mie naona awe amezibitika kisayansi baba mpya, bado hananafasi kubwa kwa mtoto!! alikuwapi tangu mtoto anazaliwa? kwa ushauri wangu baba wa zamani awe amezibitika kisansi au la!! bado anahaki yakuwa hata baba mlezi na hapo atakuwa zaidi ya baba mzazi.
 
Nashukuru sana Mkuu Mselewa nadhani nimepata mwanga juu ya swala hili na angalau nimepata pa kuanzia!
Nashukuru sana
 
Last edited by a moderator:
Mkuu kwa utaratibu wa kupima DNA watusaidie wanaoelewa zaidi, mimi napenda kuchangia kwenye upande hasa wa kijamii, kama mtoto kwa sasa ana miaka 18, na anamfahamu baba mmoja toka akiwa mtoto, nasasa kapatikana mwingine, mie naona awe amezibitika kisayansi baba mpya, bado hananafasi kubwa kwa mtoto!! alikuwapi tangu mtoto anazaliwa? kwa ushauri wangu baba wa zamani awe amezibitika kisansi au la!! bado anahaki yakuwa hata baba mlezi na hapo atakuwa zaidi ya baba mzazi.

Mkuu Kidesheni nakushukuru sana kwa Post yako imeniweka katika hatua nzuri ya kushauri juu ya swala hili naahidi ntarudisha feedback hapa!
 
Huyo aliejitokeza ana lake jambo mkuu tangu mimba hadi mtoto anakua mtu mzima anatambua baba ni L leo hii anakuja x anadai mtoto niwangu huyo atakuwa chizi tu miaka yote alikua wap? Aache kumchanganya mtoto na ninyi pia. Inashangaza watu siku hizi hawana aibu kabisa miaka 18 ndio unakuja kudai mtoto angenikuta mm nadhani angekimbia speed kumzidi bolt kwa kile ambacho ningemfanyia.
 
Ndugu wanaJF, naomba mwenye kufahamu sehemu ambayo wanatoa huduma ya kupima DNA kwa hapa tz anisaidie. natanguliza shukrani !
 
inafuatana unataka kupima kwaajili ya nini, kama ni 'kesi' mpaka upata kibali kutoka mamlaka zinazo husika kama polisi/mahakama
JIBU: kwa mkemia mkuu, jirani na hospitali ya ocen road POSTA
 
Unajua kuna vipimo vingine ktk mazingira yetu si vya lazima sana.Sasa unataka kupima DNA.. hata nimekosa cha kusema.Haya sasa umeambiwa,nenda kapime.
 
inafuatana unataka kupima kwaajili ya nini, kama ni 'kesi' mpaka upata kibali kutoka mamlaka zinazo husika kama polisi/mahakama
JIBU: kwa mkemia mkuu, jirani na hospitali ya ocen road POSTA

shukran mkuu. sasa kama unataka for parental test nayo utahitaji kuwa na kibali?
 
Ushauri wangu usiende kupima DNA potezea tu hata km unahisi mtoto si wako wewe mle utabarikiwa kwa mungu sana.
 
Nakushauri usipime. Hii ni kwa kuwa baada ya kupima DNA, utazua zogo ambalo mwisho wake litakukosesha amani. Imagine una watoto kumi, na baada ya kupima ukaambiwa watoto sita huna uhusiano nao, na awali uliamini kabisa ni watoto wako, na uliwapenda, kitu gani kitatokea.
Imagine unamwambia mtoto wako mkapime DNA, atawaza nini???? Atajiuliza, yaani baba hana imani kuwa mimi ni mtoto wake????? Yaani baba hana imani na mama?????? Yaani baba anaona mama ni m****ya????
"ISHI KWA AMANI, ACHA KUPIMA DNA"
 
anayejua na gharama ya kipimo atuwekee hapa bandugu!
 
Mi naona dai la mdau ni la msingi. Pamoja na madhara tegemewa, ila kama jamaa kuna vitu amehisi ni muhimu akavishughulikia mapema before it is too late. Sometimes you have to face the consequences badala ya kuzikwepa. Kwa hiyo mkuu wewe nenda uwe na uhakika kama unalea mwanao ama unalea wa kufikia. Na ukijua unalea wa kufikia wala usimbwage, mlee atakuja kukupa fadhila
 
mkuu achana na DNA ya kujitakia kwani inaweza kuja kukuletea matatizo makubwa sana,ila kama kuna mgogoro kwenye familia na inawalazimu kufanya hivyo basi nenda,ukikuta mambo tofauti ndugu yangu hiyo hasira utakayopata unaweza kusababisha vifo kwa hata wasio na hatia,MARA MIA KAPIME UKIMWI NA FAMILIA YAKO YOTE:msela:
 
Nilipewa taarifa miezi mitatu baada ya mtoto kuzaliwa kuwa ni wangu, kisa tu ana rangi inayofanana na mimi. Muda huo nilikuwa nimeshaoa tayari. Kwa hili ndugu KIPIMO CHA DNA NI LAZIMA. Tena wataalam tuelezeni gharama na ni wapi zaidi ukiacha kwa mkemia mkuu.
 
Back
Top Bottom