Utaratibu wa kupiga kura BUNGENI ni mbovu!! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Utaratibu wa kupiga kura BUNGENI ni mbovu!!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Inkoskaz, Apr 16, 2011.

 1. Inkoskaz

  Inkoskaz JF-Expert Member

  #1
  Apr 16, 2011
  Joined: Nov 6, 2010
  Messages: 6,318
  Likes Received: 438
  Trophy Points: 180
  Waungwana

  Utaratibu unaotumika kupitisha vifungu wakati bunge linakaa kama kamati
  haufai,speaker kuamua kwa kusikiliza sauti za ndiyo au hapana na pia wabunge kuulizwa mmojammoja inakuwa sio fair kwani sio huru kwa wabunge,wengine walazimika kusema ndivyo sivyo kwa kuepuka kupingana na misimamo ya vyama vyao

  Wadau wa sekta ya judiciary mmeona mnavyoburuziwa muswada.

  Nasema hatuna Spika na AG ni mhuni fulani tu yaani ameshindwa kutetea hoja zinazostahiki kwa wanataaluma wenzie

  Waziri wa katiba na sheria
  ndo kituko kingine...shame on them

  Mahudhurio pia ni poor sana,sasa kura za absentees zinapotea bure!

  Nawakilisha
   
 2. J

  Joshua Bukuru Member

  #2
  Apr 16, 2011
  Joined: Apr 16, 2011
  Messages: 76
  Likes Received: 68
  Trophy Points: 25
  Naomba nikujibu juu ya hoja yako hiyo hapo juu!
  Pamoja na kuwa tujibizana kupitia internet, ni vizuri na ni uungwana kutumia lugha sanifu. Asili yetu watanzania ni kwamba hata kama una chuki binafsi na mtu fulani, basi mmalize kwa hoja na si matusi. Tambua pia haya mambo yanaweza kukushtaki mahakamani. Jifunze kuwa good civilian mwenye hekima na busara.
  Ni rudi kwenye mfumo wa kupiga kura bungeni katika kupitisha maamuzi, mimi mwenyewe sikubaliani nao lakini kwa kuwa mama wa yote ni katiba, mfumo huu mbovu hauwezi kubadilika hadi pale tutakapo pata katiba huru na haki ya nchi. Mimi napendekeza kuwepo uwezo wa kupiga kura kwa njia ya masanduku na decision to pass iwe imefikia asilimia 67 ya wabunge wote waliopo bungeni. Tofauti na hivyo ni ile mbunge anapiga kura kwa kuwa bosi wake yupo pale na hii si kura ya haki kwa sababu inamnyima mtu uhuru wa kuamua ipasavyo.
   
 3. George Maige Nhigula Jr.

  George Maige Nhigula Jr. Verified User

  #3
  Apr 16, 2011
  Joined: Mar 14, 2008
  Messages: 470
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Haiwezekani wabunge wapige kura ya ku shout Ndioo au Hapanaa nadhani ni wakati sasa tufate utaratibu wa bunge la Marekani wa kupiga kura ya wazi na inakuwa recorded kuwa mbunge wa Nyamagana au bumbuli amepiga kura ya ndio au hapana na wananchi wajue jinsi mbunge wao anavyopiga kura zake na uwezo wake wa kufanya maamuzi, ili mwisho wa siku tutamuwajibisha au kumpongeza kutokana na uwezo wa mbunge wetu kufanya maamuzi.

  Wabunge wanatuwakilisha sisi wananchi tunastahili kujua mbunge wetu amepigaje kura yetu kwenye every issue kwani hivi sasa wabunge wanapiga kura ya kiholela holela tu na haziwe recorded hivyo utaratibu wa sasa sio wa kiuwajibikaji kabisa.

  Nadhani tumeona wabunge wengi hususani wa chama tawala wanapiga kura tafikiri wanajiwakilisha wao wenyewe hata hawajali kutafuta maoni ya wananchi wao wanasema nini juu ya mswaada flani au bajeti ya serikari kabla ya kupiga kura, huu ni uhuni na itabidi tupambane nao
   
 4. George Maige Nhigula Jr.

  George Maige Nhigula Jr. Verified User

  #4
  Apr 16, 2011
  Joined: Mar 14, 2008
  Messages: 470
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Bwana Joshua Bukuru,

  Napingana na wewe kuhusu hoja yako ya kupiga kura ya siri, siri ya nini wakati mbunge anamwakilisha mwananchi wake, Nadhani ni wakati muafaka tuachane na utaratibu wa kupiga kura kama waingereza za ku shout ndiooooo au Hapanaaaa, Bunge letu linahitaji kupiga kura za wazi kila mmoja ijulikane mbunge wa jimbo la Kawe kapiga kura yandio kwenye mswaada wa kupitisha bajeti na wananchi wajue mwakilishi wao kawawakilisha vipi? Nadhani utaratibu wa Bunge la marekani ni mzuri na unamfanya mbunge awajibike kwa wananchi na sio kwa special interest group kwani uwakilishi wake kwenye kupiga kura ukijulikana tutajua huyu mbunge anawakilisha wananchi wake kwa maamuzi anayofanya bungeni au anajiwakilisha yeye na chama chake au some special interest group.
   
 5. Dio

  Dio JF-Expert Member

  #5
  Apr 16, 2011
  Joined: Feb 8, 2011
  Messages: 1,278
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  Kwel kabisa mfumo mbovu.
   
 6. J

  Joshua Bukuru Member

  #6
  Apr 16, 2011
  Joined: Apr 16, 2011
  Messages: 76
  Likes Received: 68
  Trophy Points: 25
  Usemavyo ni kweli lakini bado natofautiana na wewe juu ya mfumo wa bunge tulilonalo. Umechanganya mambo mawili hapa, mfumo wa bunge la uingereza wa kupiga kura ya ndiyo au hapana na mfumo wa bunge la marekani ambapo kila hoja iliyopo mezani lazima ipigiwe kura ya wazi ili kuunga mkono. Bahati mbaya ni kwamba Tanzania tunafuata mfumo wa uingereza na ndiyo maana zomea zomea inasikika kwenye maamuzi muhimu yenye mustakabali wa taifa. Mbali na hiyo, wabunge wetu si wawakilishi wa wananchi bali vyama vyao vya siasa, ukitaka kuelewa kuwa hili ni kweli, mbunge atofautiane na chama uone kitakachotokea. Binafsi natamani mfumo wa marekani, ukishachaguliwa unaitwam mwakilishi wa watu na hata kama unge kitukana chama chako, hupotezi sifa za kuwa mbunge. Uzuri wa yote ni kwamba, tupo kwenye mchakato wa katiba mpya, tulipigie kelele hili liingizwe kwenye katiba. Kutakalika bungeni?
   
 7. Inkoskaz

  Inkoskaz JF-Expert Member

  #7
  Apr 16, 2011
  Joined: Nov 6, 2010
  Messages: 6,318
  Likes Received: 438
  Trophy Points: 180
  mkuu nakubaliana nawe ila yale yaliokuwa yakifanyika ni uhuni na ndio maana aliyekuwa akiongoza kupiga chini hoja nzuri nikampa stahiki ya cheo kinachofanana na hicho alichokua akikifanya mbele ya waTZ
  binafsi sina chuki na werema but alichokuwa anafanya kimetuumiza waTZ wengi ukiwamo wewe pia unayemuona muungwana
   
 8. Inkoskaz

  Inkoskaz JF-Expert Member

  #8
  Apr 16, 2011
  Joined: Nov 6, 2010
  Messages: 6,318
  Likes Received: 438
  Trophy Points: 180
  good observation mkuu umenena
   
Loading...