Utaratibu wa kuomba ruhusa katika utumishi wa umma

Adjussi

Member
May 25, 2014
39
15
Habari zenu wakuu.

Kwa mwenye ufahamu naomba kujuzwa hivi mtumishi wa umma kwa mwaka anatakiwa kuomba ruhusa jumla siku ngapi?na je kwa watumishi wanaochukua/kuomba ruhusa mara kwa mara utaratibu ukoje wa kuwadhibiti?

Natanguliza Shukrani.
 
siku 14 ndiyo mwisho wa ruhusa.Akiomba ruhusa nyingine baada ya kuwa ametumia hizo siku 14 inabidi siku hizo atakazoruhusiwa zikatwe kutoka katika likizo yake ya mwaka. Kwa hiyo wakati wa likizo ataenda siku pungufu ya 28.
 
Mtumishi ana siku 56 kwa mwaka. 28 likizo ambayo ni annual leave aingiliwi na suala lingine na 28 za ruhusa ya matatizo mbali mbali misiba kuuguza homa nk.nk
Tafuta standing order itakupa muongozo
Idumu amani ya Tanzania.
 
Ukiomba ruhusa zaidi ya siku 5 lazima watakuandikia kuwa zitakatwa kwenye likizo yako.Wengi huwa tunaomba 5/4 then ukiweza unavuta kiaina ili kukamilisha kisababishi cha ruhusa
 
Back
Top Bottom