Utaratibu wa kumuachisha mtu kazi

fimboyaasali

JF-Expert Member
Jan 14, 2011
8,377
7,896
Naomba wajuzi wanifahamishe iwapo unataka kumuachisha mtu kazi, na iwapo hajaenda likizo miaka 5 unapotengeneza mafao yake unaingiza na malipo ya likizo zote 5?
 
Naomba wajuzi wanifahamishe iwapo unataka kumuachisha mtu kazi, na iwapo hajaenda likizo miaka 5 unapotengeneza mafao yake unaingiza na malipo ya likizo zote 5?

Cha kwanza lazima nifahamu je ulimpa mkataba wa aina gani maana Sheria ya ajira na mahusiano kazini 2004 kifungu cha 14 kinasema mkataba unaweza kuwa wa 1. muda maalumu 2. kazi maalumu 3. mkataba usio na muda maalumu

Tukishajua hilo lazima pia kufahamu je ulikuwa unamlipaje kila mwezi maana Minimum wage order 2013 inaweka wazi kima cha chini cha kumlipa mfanyakazi ambacho kila sekta ipo hapo ila kama ilikiuka hapo ilo tatizo

Je ulikuwa unamchangia katika mfuko wa jamii NSSF maana kama ulikiuka NSSF ACT 1997 haiwezi kukuacha salama maana kifungu cha 14 kinasema upigwe faini ya asilimia 5 kila mwezi ambapo hukupeleka mchango

MKATABA UNAWEZA KUKOMA KWA, hii ipo kifungu cha 36 Sheria ya ajira na mahusiano kazini 2004 inasema 1. makubaliano 2. mfanyakzi kujiuzuru 3. kuisha kwa mkataba

SABABU AMBAZO ZINAWEZA KUTAMBULIKA NI HALALI MBELE YA SHERIA KUMUACHISHA MTU KAZI
HII ipo kifungu cha 37

1. uwezo mdogo yani kufanya kazi chini ya kiwango
2. kupunguza wafanyakazi sababu za kiundashaji
3. Utovu wa nidhamu
4. kushindwa kuendana

ANGALIZO kila sababu hapo ya kumuachisha mtu kazi ina hatua na utaratibu wake kutokana na CODE OF GOOD PRACTICE 2007 yani kiswahili inaitwa KANUNI ZA AJIRA NA MAHUSIANO KAZINI

TUJE SASA STAHIKI UNAZOTAKIWA KUMLIPA
hii inapatikana kwenye sheria ya ajira na mahusino kazini 2004 KIFUNGU CHA 44 yani wanaita TERMINAL BENEFITS

1. unatakiwa kumlipa mshahara wa siku alizofanya kazi
2. Likizo ya mwaka huu siku 28
3. likizo zote za nyuma ambazo hakuwahi kuchukua
4. Unatakiwa kumlipa taarifa ya kumfukuza yani notice ya siku 28
5. Kiinua mgongo cha miaka 5 na kinapigwa hesabu hivi mfano mshahara wa siku ni 10,000 utafanya hivi = 10,000*7*5 yami mshahara wa siku kwa muda wa siku 7 kwa idadi ya miaka aliyofanya kazi
6. Kama ulimtoa shinyanga ukamleta dar itabidi umlipe nauli ya kurudi shinyanga

no 7 hii ndo ngumu kumeza kwa kuwa wewe ndo umtaki mfano mktaba ulitakiwa uishe mwezi wa 12 wewe mwezi wa pili ndo umesema humtaki mahakama itakuradhimu ulipe mshahara wa miezi 10


ushauri wangu

KUNA DOCUMENT INAITWA MUTUAL TERMINATION AGREEMENT AND DISPUTE SETTLEMENT KAA NAE CHINI MUELEWANE ALAFU AWEKE SAHII KWENYE HIYO DOC NA KIWANGO CHA PESA UNACHOTAKIWA KUMLIPA ALAFU MLIPE ATAWEKA NA KIDOLE GUMBA NA ULE WINO BAADA YA HAPO MPE NAKALA MOJA HATA AENDE POPOTE UTAKUWA UPO SALAMA
 
Back
Top Bottom