Shukrani A. Ngonyani
JF-Expert Member
- Feb 23, 2014
- 1,179
- 2,004
Rais hapatikani kwa bahati mbaya, hupitia mchujo ktk chama chake, ktk tume ya uchaguzi na hatimaye ktk box la kura kwa wananchi.
Mimi si mtaalamu wa sheria, ni mbumbumbu ktk hii field ya sheria, ninachofanya hapa ni kuchokoza, wenye kujua wahamaki, wajadili hivyo lengo ni kuibua mjadala.
Utaratibu wa kumpata mgombea urais na kumpata rais kwa ujumla wake uko vibaya sana, umejaa mapungufu mengi. na hata mfumo wa kumwajibisha rais umekuwa na kasoro nyingi sana pia.
Wananchi Waliomchagua rais laziwa wawe na uwezo wa kumtoa rais pale anaposigina katiba au anaposhindwa kuongoza vyema.
Athari ya kumpata rais ambaye hakuandaliwa vyema ni kubwa, na madhara ya kuendelea kumwacha madarakani rais anayevuruga nchi ni kubwa pia.
Ufanyike mjadala wa kikatiba, rais apatikane akiwa amepimwa vyema uadilifu wake, maadili yake, historia yake, busara na uvumilivu wa kisiasa na hata mwenendo wa familia yake.
Nafasi ya urais sio by chance, eti wawili waliostahili wakagombana, huyu watatu akapita kwa udhaifu huo.
Rais akiwa madarakani pia aondolewe hata kwa petition tu na ikibidi kwa kuwa tulimpima kwa busara hapo mwanzoni, awe tayari kujiuzulu pale wengi wanapolalamikia utawala wake.
Unahitajika mjadala wa kikatiba, hapo juu nimetahadharisha kuwa mimi ni mbumbumbu wa sheria, hapa nachokoza ili wajuzi wa sheria wahamaki, wajadili na hatimaye kuwe na mjadala wa kikatiba.