Utaratibu wa kumpata na kumwondoa Rais pamoja na kumwajibisha akiwa madarakani ufanyike

Shukrani A. Ngonyani

JF-Expert Member
Feb 23, 2014
1,179
2,004
Rais hapatikani kwa bahati mbaya, hupitia mchujo ktk chama chake, ktk tume ya uchaguzi na hatimaye ktk box la kura kwa wananchi.

Mimi si mtaalamu wa sheria, ni mbumbumbu ktk hii field ya sheria, ninachofanya hapa ni kuchokoza, wenye kujua wahamaki, wajadili hivyo lengo ni kuibua mjadala.

Utaratibu wa kumpata mgombea urais na kumpata rais kwa ujumla wake uko vibaya sana, umejaa mapungufu mengi. na hata mfumo wa kumwajibisha rais umekuwa na kasoro nyingi sana pia.

Wananchi Waliomchagua rais laziwa wawe na uwezo wa kumtoa rais pale anaposigina katiba au anaposhindwa kuongoza vyema.

Athari ya kumpata rais ambaye hakuandaliwa vyema ni kubwa, na madhara ya kuendelea kumwacha madarakani rais anayevuruga nchi ni kubwa pia.

Ufanyike mjadala wa kikatiba, rais apatikane akiwa amepimwa vyema uadilifu wake, maadili yake, historia yake, busara na uvumilivu wa kisiasa na hata mwenendo wa familia yake.

Nafasi ya urais sio by chance, eti wawili waliostahili wakagombana, huyu watatu akapita kwa udhaifu huo.

Rais akiwa madarakani pia aondolewe hata kwa petition tu na ikibidi kwa kuwa tulimpima kwa busara hapo mwanzoni, awe tayari kujiuzulu pale wengi wanapolalamikia utawala wake.

Unahitajika mjadala wa kikatiba, hapo juu nimetahadharisha kuwa mimi ni mbumbumbu wa sheria, hapa nachokoza ili wajuzi wa sheria wahamaki, wajadili na hatimaye kuwe na mjadala wa kikatiba.
 
Any fool can criticize, complain, and condemn—and most fools do. But it takes character and self-control to be understanding

hatuwezi kuigeuza nchi yetu kichaka cha wapiga deal hata siku moja mlikuwa mmeshatufikisha kubaya ni ukweli usiofichika kuwa watanzania wengi maisha yenu mlikuwa mnayaendesha kwa fedha haramu na yalikuwa ni maisha ya House of Cards ambayo si Stable wapiga deal walikuwa wanasababisha inflation kubwa sana walikuwa wanasababisha mpaka interest rates kufikia 21.42% kiwango cha juu kabisa kuwai kutokea kwa nchi ambayo hakuna tatizo lolote na infalation ilifikia 5.6% ilifikia Temeke nyumba ambayo uwezi kuishi sana sana utaivnja tu yani ni kiwanja tu walikuwa wanauza milion 500 kweli?? na wanunuzi wanapigana vikumbo kununua

vyumba mpaka Tabata unalipa rent kwa dola kweli na watu wala awalalamiki na hiyo yote kwa sababu milikuwa mnazo ela za kulipa leo ukienda Canada ukawekeza kiwango cha kuanzia dola 100,000 tu ukiomba Permanent residency wanakupa lakini eti Tanzania eti dola laki moja mtu kampangishia kimwana na hyo ni kodi ya mwaka mikocheni kweli???

Kila mwaka ada za watoto zinapanda mtu analipa milion 3 kwa mwaka mtoto anasoma shule ya msingi uwezi kuona hatari kwa vile unayo ela ya kulipa sasa mashule hayo ya ada milion 3 yakkosa wanafunzi kwa sbabu watu awana ela ya kulipa watashusha wenyewe ada wanasema thamani ya kitu au bidhaa uamuliwa na nguvu ya soko
Watanzania tulikuwa tumefikia nchi yetu kuipeleka kubaya tofauti yetu na Zimbabwe ambapo mtu ananunia fungu la dagaa kwa sh 10000 likuwa ni zimbabwe kuna vikwazo vya uchumi lakini sisi hatuna na ndo tulikuwa tunakwenda huko value of money ilikuwa inakwenda kupotea kabisa
 
Rais hapatikani kwa bahati mbaya, hupitia mchujo ktk chama chake, ktk tume ya uchaguzi na hatimaye ktk box la kura kwa wananchi.

Mimi si mtaalamu wa sheria, ni mbumbumbu ktk hii field ya sheria, ninachofanya hapa ni kuchokoza, wenye kujua wahamaki, wajadili hivyo lengo ni kuibua mjadala.

Utaratibu wa kumpata mgombea urais na kumpata rais kwa ujumla wake uko vibaya sana, umejaa mapungufu mengi. na hata mfumo wa kumwajibisha rais umekuwa na kasoro nyingi sana pia.

Wananchi Waliomchagua rais laziwa wawe na uwezo wa kumtoa rais pale anaposigina katiba au anaposhindwa kuongoza vyema.

Athari ya kumpata rais ambaye hakuandaliwa vyema ni kubwa, na madhara ya kuendelea kumwacha madarakani rais anayevuruga nchi ni kubwa pia.

Ufanyike mjadala wa kikatiba, rais apatikane akiwa amepimwa vyema uadilifu wake, maadili yake, historia yake, busara na uvumilivu wa kisiasa na hata mwenendo wa familia yake.

Nafasi ya urais sio by chance, eti wawili waliostahili wakagombana, huyu watatu akapita kwa udhaifu huo.

Rais akiwa madarakani pia aondolewe hata kwa petition tu na ikibidi kwa kuwa tulimpima kwa busara hapo mwanzoni, awe tayari kujiuzulu pale wengi wanapolalamikia utawala wake.
TUNASUBIRI AMALIZE 10 TUMUONGEZEE MINGINE.
 
Any fool can criticize, complain, and condemn—and most fools do. But it takes character and self-control to be understanding

hatuwezi kuigeuza nchi yetu kichaka cha wapiga deal hata siku moja
Wapiga dili wale waliobeba noti kwenye viroba au wapiga dili gani? Au wale walituambia dangote anataka Gas bure au wapiga dili gani wengine? Na Ile mahakama ya mafisadi vipi imekosa washtakiwa kwahiyo mmeshindwa kuwafikisha mahakamani wapiga dili?

Anaeweza kukuubaliana na wewe lazima awe anatoka ukoo wa kijani tu
 
Toka serikali hii umemsikia nani kabeba fedha kwenye viroba???? usilete mifano ya mwaka 2015 kurudi nyuma tunazungumzia serikali hii ambayo muda wake ni mpaka 2020 wakichukuliwa hatua mnakuja hapa na Id fake kuja kupinga na kusema wameonewa tukubali tukatae wapga deal mko na hali mbaya sana mmebanwa kila kona na swala la Gesi limeshakwisha na Dangote mwenyewe kasema siku ile kuwa hakuna tatizo na analeta trucks 600
 
Nnacho pendea nchi za wenzetu ni kwamba rais anaanfaliwa toka akiwa mtoto!! Waangalie akina putin..afu mcheki PM wa israel netanyahu!! Sasa ukija huku kwetu mambo ni tofauti kabisa
 
Rais hapatikani kwa bahati mbaya, hupitia mchujo ktk chama chake, ktk tume ya uchaguzi na hatimaye ktk box la kura kwa wananchi.

Mimi si mtaalamu wa sheria, ni mbumbumbu ktk hii field ya sheria, ninachofanya hapa ni kuchokoza, wenye kujua wahamaki, wajadili hivyo lengo ni kuibua mjadala.

Utaratibu wa kumpata mgombea urais na kumpata rais kwa ujumla wake uko vibaya sana, umejaa mapungufu mengi. na hata mfumo wa kumwajibisha rais umekuwa na kasoro nyingi sana pia.

Wananchi Waliomchagua rais laziwa wawe na uwezo wa kumtoa rais pale anaposigina katiba au anaposhindwa kuongoza vyema.

Athari ya kumpata rais ambaye hakuandaliwa vyema ni kubwa, na madhara ya kuendelea kumwacha madarakani rais anayevuruga nchi ni kubwa pia.

Ufanyike mjadala wa kikatiba, rais apatikane akiwa amepimwa vyema uadilifu wake, maadili yake, historia yake, busara na uvumilivu wa kisiasa na hata mwenendo wa familia yake.

Nafasi ya urais sio by chance, eti wawili waliostahili wakagombana, huyu watatu akapita kwa udhaifu huo.

Rais akiwa madarakani pia aondolewe hata kwa petition tu na ikibidi kwa kuwa tulimpima kwa busara hapo mwanzoni, awe tayari kujiuzulu pale wengi wanapolalamikia utawala wake.

Unahitajika mjadala wa kikatiba, hapo juu nimetahadharisha kuwa mimi ni mbumbumbu wa sheria, hapa nachokoza ili wajuzi wa sheria wahamaki, wajadili na hatimaye kuwe na mjadala wa kikatiba.

Ni kweli kabisa,kama Taifa tunatakiwa tuwaandae watu kwenye nafasi hii nyeti siyo iwe ya kuchaguliw amaadui na marafiki.Hatuwezi kuwa na MARAIS ambao wanapa kuilinda KATIBA halafu wanakuwa wakwanza kuikanyaga,wanaapa kutuongoza kama TAIFA lakini wanatubagua kwa ITIKADI zetu,wanaatubagua hata kwenye ajira,hakika tunahitaji KATIBA itakayotupa HAKI RAIA kuamua mustakabali wa TAIFA letu,tusiwaachie watu ambao hata huko nyuma tulizijua HULKA na TABIA zao
 
Rais hapatikani kwa bahati mbaya, hupitia mchujo ktk chama chake, ktk tume ya uchaguzi na hatimaye ktk box la kura kwa wananchi.

Mimi si mtaalamu wa sheria, ni mbumbumbu ktk hii field ya sheria, ninachofanya hapa ni kuchokoza, wenye kujua wahamaki, wajadili hivyo lengo ni kuibua mjadala.

Utaratibu wa kumpata mgombea urais na kumpata rais kwa ujumla wake uko vibaya sana, umejaa mapungufu mengi. na hata mfumo wa kumwajibisha rais umekuwa na kasoro nyingi sana pia.

Wananchi Waliomchagua rais laziwa wawe na uwezo wa kumtoa rais pale anaposigina katiba au anaposhindwa kuongoza vyema.

Athari ya kumpata rais ambaye hakuandaliwa vyema ni kubwa, na madhara ya kuendelea kumwacha madarakani rais anayevuruga nchi ni kubwa pia.

Ufanyike mjadala wa kikatiba, rais apatikane akiwa amepimwa vyema uadilifu wake, maadili yake, historia yake, busara na uvumilivu wa kisiasa na hata mwenendo wa familia yake.

Nafasi ya urais sio by chance, eti wawili waliostahili wakagombana, huyu watatu akapita kwa udhaifu huo.

Rais akiwa madarakani pia aondolewe hata kwa petition tu na ikibidi kwa kuwa tulimpima kwa busara hapo mwanzoni, awe tayari kujiuzulu pale wengi wanapolalamikia utawala wake.

Unahitajika mjadala wa kikatiba, hapo juu nimetahadharisha kuwa mimi ni mbumbumbu wa sheria, hapa nachokoza ili wajuzi wa sheria wahamaki, wajadili na hatimaye kuwe na mjadala wa kikatiba.

You think Great brother!

Katika shajara na Nelson Rolinhahla Mandela cha LONG WALK TO FREEDOM anasema kuwa "Kiongozi mzuri hupimwa kwa namana alivyo na mahusiano mazuri na wananchi wake wa chini na siyo wananchi wa juu",Viongozi wetu wako hivyo and we need to think beyond.

Kunahitajika mijadala ya Nguvu katika hili.
 
Back
Top Bottom