Utaratibu wa kula chakula mezani

mfianchi

Platinum Member
Jul 1, 2009
11,855
8,251
Nakumbuka nilipokuwa mdogo mama yangu alikuwa ameweka miiko wakati wa kula chakula,na alikuwa mkali kwelikweli pale inapokuwa tunakiuka hiyo miiko,lazima utafinywa kwenye mashavu.
Moja ya miiko mikubwa alituambia tunapokula chakula tule taratibu na huku umefunga mdomo,hilo linapunguza kwa kinyakyusa tunaita ulugaju yaani kelele za kutafuna chakula zinnapotoka mdomoni inakuwa kama vile nguruwe anakula miwa au machicha,pia kutozungumza wakati unakula hiyo inapunguza kupaliwa au kukohoa ambapo hatima yake unaweza ukatoa chakula kutoka mdomoni na kikawangukia wengine,kwa hilo namshukuru sana mama yangu the Iron lady.Kwa siku hizi napigwa na butwaa ninapomuona mtu mzima akila chakula huku domo liko wazi na ule msago wa chakula ukisikika mpaka nje,jamani tujifunze ustaarabu wa kula chakula na pia tuwafundishe vijana wetu,hata kula njiani vitu kama mahindi au matunda si ustaarabu
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom