Utaratibu wa kujiunga na JKT 2014 kwa wahitimu Kidato cha VI

nngu007

JF-Expert Member
Aug 2, 2010
15,862
5,797
UTARATIBU WA KUJIUNGA NA JESHI LA KUJENGA TAIFA VIJANA KWA MUJIBU WA SHERIA WANAOMALIZA KIDATO CHA SITA MEI 2014.


  • AWAMU YA KWANZA; Vijana 20,000 wataripoti kwenye makambi ya mafunzo ya JKT kuanzia tarehe 01 Juni 2014 na kuanza rasmi mafunzo yao tarehe 08 Juni 2014 na kumaliza tarehe 04 Septemba 2014. Orodha yao itaanza kuonekana kwenye websiteya JKT tarehe 11 Mei 2014 kuanzia saa nne (4) asubuhi.

  • AWAMU YA PILI; Vijana 14,450 wataripoti kwenye makambi ya mafunzo ya JKT kuanzia tarehe 11 Septemba 2014 na kuanza rasmi mafunzo tarehe 18 Septemba 2014 na kumaliza tarehe 17 Desemba 2014. Orodha yao itaanza kuonekana kwenye website ya JKT tarehe 15 Mei 2014 kuanzia saa kumi (10) jioni.

  • Kijana yeyote mwenye ulemavu unaoonekana aripoiti katika kambi ya mafunzo ya Ruvu JKT (832 Kikosi cha Jeshi).

  • Vijana wote wanatakiwa kuwa na vyeti vya kumaliza Kidato cha Sita (Leaving Certificate).


  • Inasisitizwa vijana waripoti kwenye makambi waliyopangiwa na siyo kuja Makao Makuu ya JKT.

Bofya majina ya makambi yaliyopachikwa hapo chini kupakua na kufungua ukurasa kuona majina ya walioitwa katika Awamu ya Kwanza.


  1. BULOMBORA - KIGOMA
  2. RWAMKOMA - MUSOMA
  3. MSANGE - TABORA
  4. KANEMBWA - KIGOMA
  5. RUVU - PWANI
  6. OLIJORO - ARUSHA
  7. MGAMBO KABUKU - TANGA
  8. MARAMBA - TANGA
  9. MAFINGA - IRINGA
  10. MLALE - SONGEA
  11. MTABILA - KIGOMA
  12. MAKUTOPORA - DODOMA

Kwa ufafanuzi zaidi wasiliana na info@jkt.go.tz



Taarifa hii imetolewa na:
Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa.
via www.jkt.go.tz

Chanzo:
Wavuti
 

Nyerere was GENIUS - This PLAN will not hold water... !!!
 
Inaamaana hawa awamu ya 2 chuo hawataenda na badala yake wataenda kuruka vichura kutukanwa na kulambishwa mchanga huko makambini?
 
Tupeni maelezo zaidi na wale wa awamu ya pili..na nasikia kwamb wataenda after chuo?? maelezo mkubwa uliye toa maada hapo juu ..quote ninngu 077
 
usijali kandudi...awamu ya pili ni kama kaka zenu mwaka jana, mtaendelea kusubir until further notice
 
Back
Top Bottom