Utaratibu wa kufungua kesi mahakamani kwa makosa ya barabarani

GreatMkubwa

Member
Jun 25, 2012
99
57
Habari za leo wadau. Naomba wenye uelewa wa namna ambavyo naweza kulalamika pale ambapo askari wa barabarani kanilazimisha kuandika fine bila ya mimi kuridhia kosa langu.
Nimewahi kukutana na mikasa mingi ya askari barabarani mpaka inafikia mahali nahisi labda kuna mambo siyafahamu au basi tuu ni ubabe wa askari.
1. Leo asubuhi sana majira ya saa kumi na mbili kasorobo nimesimamishwa na askari kwa kosa la kuovertake mahali ambapo sio salama. Gari ziliongozana nyingi na alisimamisha gari langu ambapo haikuwa gari sahihi, akaniambia umeovateki pale, nikamwambia wapi? akaanza kufoka na kudai ninamchalenge na ameona nikiovateki, mwenzie akamwambia mwandikie huyo akalalamike popote aende hata mahakamani.
enewey akaandika, nikapokea na kuendelea na safari zangu.
2. Kuna siku pia askari alishanisimamisha maeneo yenye taa za barabarani akidai nimepita kwenye red light nikamwambia hapana, iliwaka wakati namalizia, ofcoz ilikuja njano nikiwa katikati ya kumaliza eneo la taa, tulibishana mda mrefu badae akaniacha niende.
3. Zipo habari za tochi zinapigwa na unaonyeshwa picha mbele huko, sometimes mpigaji kajificha mahali hamna 50kmph ya kuanzia ila ipo ya kumalizia

Yote juu ya yote naomba mwenye uelewa wa ziada katika haya mambo. Nina experience ya kutosha katika udereva ila yapo mambo yananitatiza everyday.
1. Nafunguaje kesi?
2. Ushahidi wa kuovertake unapatikanaje?
3. Je nitapata haki yangu?
 
Pole Mkuu, haki unayo na utaratibu ni kugoma kulipa fine yao ili ukishashtakiwa ukate rufaa ila kinyume na hapo hautaweza kupata haki yako kwa mtu anayelazimisha raia mwema kuwa mshtakiwa.
 
Pole Mkuu, haki unayo na utaratibu ni kugoma kulipa fine yao ili ukishashtakiwa ukate rufaa ila kinyume na hapo hautaweza kupata haki yako kwa mtu anayelazimisha raia mwema kuwa mshtakiwa.
Mara nyingi hayo makosa ya KU overtake sehemu isiyo sahihi na tochi huwa traffic hawaonei kwa uzoefu wangu wanakuwa sahihi kabisa.Kuna wale wasiosimama eneo la Zebra Aisee pale mnazi mmoja soko la kisutu Askari huwa wanawadaka madreva Kama kuku wa mdondo kwa kutosimama zebra wanakula vichwa hasa.Hawana uonezi mleta mada Ni wale madereva wakorofi tu wa barabarani ambao akiwa barabarani na kigari chake used huwaona matraffic Kama malofa Fulani tu.
 
nimemuona huyu,badala ya kuomba msaada wa kisheria anashitaki na mengine ambayo yamepita.
 
YEHODAYA
Ingependeza kama nikipata majibu ya swali langu, pia sio sahihi saana kuwaza kuwa woote wanaoambiwa wametenda kosa wamelitenda kweli!! Sometimes uonevu upo, pia hao trafiki unaosema nimewaona kama malofa - una uhakika? I always respect people na kazi zao sana. Usijibu kama huna majibu.
 
Back
Top Bottom