Utaratibu wa kufundishwa mambo, je ulianza lini, nani aliuanzisha, ulianzia wapi?

kendy

JF-Expert Member
Apr 30, 2015
266
494
Kitendo cha kufundisha kipo toka enzi na enzi,kila mzazi ama mtu mzima huwafundisha watoto ama wadogo zao jinsi ya kutenda ,kufanya ama kutekeleza jambo fulani kwa utaratibu uleule.
Sasa je ,ni nani aligundua utaratibu wa kuwakusanya watu wazima ama watotot wadogo na kuanza kuwafundisha mambo kwa utaratibu maalumu,kwa kutumia syllabus au mitaala, kwa mtindo wa kwenda shuleni kwa pamoja na kurudi nyumbani na kisha kesho kwenda tena ,ama kukaa shule hadi mtu anahitimu na kutunukiwa cheti ama vinginevyo.
Utaratibu wa kufundishwa mambo ( kupewa elimu)kwa kwenda kufundishwa shuleni ni utaratibu uliosambaa dunia nzima kwa sasa,je ulianza lini,nani aliuanzisha,ulianzia wapi.
 
Huo utaratibu ulianza miaka ya 800 na kuendelea kabla ya kuzaliwa kristo,

Ilikua ni kipindi ambacho falme (empire) zilianza kutokea, wafalme waliishi kwa kutegemea kodi (mazao), au kuvamia falme zingine na kupora mazao kisha kugeuza falme hizo kuwa sehemu zao

Idadi ya watu iliongezeka kwa kasi, haikuwa rahisi kutambua nani kalipa Jodi na nani hajalipa, ndipo hapo ulipoanzishwa utaratibu wa kubuni alama ambazo zilichorwa ktk kibao kilichotengenezwa kwa udongo wa mfinyanzi, kila mtu aliyetoa Jodi aliorodheshwa hapo waliweza kutunza kumbu kumbu, miaka ilivyokua mingi wakajikuta vibao ni vingi sana pia wanahitaji watu/ wasaidizi wengi,

Ndipo hapo wakaanza kuwafundisha baadhi ya watu wachache ambao walikua watoto wa wafalme n.k, walijikuta wanatengeneza formula mbali mbali na namna ya kuhifadhi masijala

Ilikua ni huko babeli, baadae Huo mfumo ukafanyika misri, China kisha ukaenea sehemu mbali mbali
 
Wazo lilikuwa zuri, walianza kukosea walipoongezea kitu MTIHANI, kimeninyanyasa Sana kwenye maisha haya mafupi!
 
Wazo lilikuwa zuri, walianza kukosea walipoongezea kitu MTIHANI, kimeninyanyasa Sana kwenye maisha haya mafupi!
Kwa taarifa yako,

Shule zote pamoja na vyuo vikuu, zilianzishwa ili kutengeneza wafanya kazi ktk taasisi kubwa kama vile serikali na makampuni ya wafanya biashara wakubwa,

Kwa mfano ili uweze kuviona vijidudu wa typhoid ktk kinyesi cha binadamu utahitaji maabara nzuri yenye vifaa kama vile hadubini, vipande vidogo vilivyotengenezwa kwa kioo pamoja na kemikali mbali mbali, hivyo vitu vyote vinahitaji pesa,
Wafalme na wafanya biashara waliwafadhili watu mbali mbali wafanye utafiti ktk mambo ambayo yatawaletea faida zaidi kama vile kuvumbua migodi ya dhahabu n.k.

Kupitia tafiti kama hizo maarifa mbali mbali yalivumbuliwa, ndiyo haya tunayoyasoma mashuleni
 
Back
Top Bottom