Utaratibu wa kuendesha nchi kisiasa hauna mafanikio!! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Utaratibu wa kuendesha nchi kisiasa hauna mafanikio!!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Anold, Aug 11, 2011.

 1. A

  Anold JF-Expert Member

  #1
  Aug 11, 2011
  Joined: Jul 15, 2010
  Messages: 1,380
  Likes Received: 300
  Trophy Points: 180
  Hili ni swali ambalo ninajiuliza kila wakati, huenda hata wewe umeshajiuliza au unaweza kujiuliza kuwa hivi haiwezakani utaratibu mwingine wa kuongoza nchi ukabuniwa na kusabababisha nchi ijiendeshe kisayansi?

  Haya mambo ya siasa siasa naona kwa nchi hasa za kiafrika yameleta matatizo makubwa na sidhani kama yameeleweka vizuri kwa sisi waafrika, ingekuwa nchi ni kampuni nafikiri haingetuchukuwa muda kutafuta mtaalam mwelekezaji ili ajaribu kutuelekeza nini cha kufanya ili tunasuke kwenye hali duni za maisha tulizo nazo.

  Kilio kikubwa cha wananchi ni kutaka kuboreshewa hali zao za maisha na unapozungumzia hali za maisha unazungumzia uchumi kwa ujumla wake ambao ili kufanikiwa kwenye eneo hilo ni lazima kanuni zinazotawala kwenye eneo la uchumi zitumike.

  Shida ninayopata ni kuona kuwa kwenye eneo kama hilo kunaingizwa siasa!!!! Mfano msuri tu kunasiku tuliambiwa Kilimo kwanza, wakati tamko hilo linatolewa hakuna hata utafiti uliofanyika kujua kuwa hicho kilimo kwanza kinafanywa na nani, lini na wapi. Mwanasiasa alisimama akasema kilimo kwanza wakati mlimaji hana taarifa! hiyo ni siasa.

  Ilitokea siku fulani tukaambiwa maisha bora kwa kila mtanzania!! sasa jamani haya mambo nashindwa hata kuyaeleza vizuri hapa, maana kauli kama hiyo "maisha bora kwa kila mtanzania" imejikita kweli kwenye sababu za kisanyansi na utafiti pamoja na hali halisi?

  Haya mambo ya siasa za kutafuta kupigiwa makofi majukwaani kama hayataaangaliwa kamwe hakuna siku hata ipite mika 1000 ikatokea nafuu kwa mwananchi. Nafikiri ifike siku viongozi wetu watenganishe siasa na mambo ya kiutendaji yanayohitaji wataalam wanaotumia taratibu zinazoeleweka zinazoweza kutuondoa kwenye porojo za kiasiasa.

  Huko tuendako nafikiri ifike siku ibainishwe vizuri kuwa ni mtu wa aina gani anahitakiwa agombee kiti cha uongozi, awe na elimu na utaalam gani n.k. sasa hivi ni tofauti ukisikia Profesa anagombea Nafasi ya uongozi ujue hana anachotafuta zaidi ya kwenda kuiga mambo ya siasa na kutupilia taaluma yake mbali.

  Kwa nchi za Afrika nafikiri inabidi siasa zipewe nafasi ndogo sana vinginevyo tutakuwa watu wa kupewa misaada na kudhurumiwa mali zetu huku wenyewe tusijue kinachoendelea
   
Loading...