Utaratibu wa kuendesha ""atcl na trl"" kwa kodi umefika mwisho sasa!!! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Utaratibu wa kuendesha ""atcl na trl"" kwa kodi umefika mwisho sasa!!!

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Pdidy, Feb 22, 2011.

 1. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #1
  Feb 22, 2011
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 33,586
  Likes Received: 5,772
  Trophy Points: 280
  Waziri wa mawasiliano na uuchukuzi amenukuliwa na vyombo vya habari akisema serikali imekuwa aikilipa mishahara ya wafanyakazi wa atcl na trl kwa kupitia kodi za wananchi na kusema sasa imefika kikomo ..akiongea kwa hisia mh wazifri amesema aiwezekani mashirika makubwa kama haya ata ukimleta mtu toka marekani umwambie ati yameshindwa kujiendesha kabisa na sasa yako taabani... Mh waziri amesema kuna mashirika ya ndeege yameanza juzi juzi tu na hayana hata miezi kadhaa yanapasua anga kila sehemu na kubeba abiria ambao wangekuwa wakibebwa na atcl.na sasa wameanza kutafuta safari za kwenda nje..hii ni moja ya maendeleao..na dhan sasa umefika wakati kuwapa kipaumbele mashirika yatakayotoa msaada wa anga na reli aijalishi ni shirika gani..aiwezekani serikali inalipa watu mishahara ya atcl na trl zaidi ya miaka mitatu..tumeingia tunaangalia makabrasha unatikisa kichwa kabla ujamalizia jinsi mamillion yanavyopelekwa kwenye mashirika haya.na bado yako taabani..kuna haja ya kusaidia hata haya ya watu binafsi yamkini tuwe na uhakika usafiri wa anga ukow akati wote,,wa tren tunaangaika kutafuta mtu wa kuchukua shirika hili ingawa kweli ni ngumu ..na hali si shwari..ila serikali inafanya iwezavyo kuyanasua mashirika haya ..ila kwa upande wangu naona imefika wakati kwa serikali kuwa tegemezi ya mishahara ya mashirika haya alisema mh waziri

  kwako mh waziri
  tunatambua serikali ina wajibu wa kusimamia mashirika haya ktk mchakato wa kuyageuza akuwa mashirika ya kujitegemea yanayojiendehsa yenyewe.. Kwa miaka mingi sasa imeshindikana kikubwa kinachojitokeza kila siku niahadi hewa zisizoisha

  trl na atcl ni masalia tu ya misusruru ya makampuni ya umma yaliokwisha jiondoa kwenye ulimwengu wa kujiendesha kibiashara yalikwisha funga shuguli zake siku nyingi.. Na kutegemea ruzuku serikalini

  ukitafakari kwa makini uwezi elewa kwa kina mfano ni kwa nini atcl na trl yameshindwa kujiendesha??kwa ufanisi. Na kushindwa kupata faida ya kuweza kijikimu na mahitaji yake..kama kulipa kodi za serikali,kulipa mishara ya wafanyakazi,kuwekeza na kweli kuweza kugawa hisa kwa wanahisa kwenye mgao wake..ni vigumu kuelewa kwa kuwa sekta walizijikita kuna shuguli zakutosha sana kibiashara tena biashara ya mabilion kwa mwezi..

  Tukiweka pembeni trla inakuwa vigumu kuelewa atcl inashindwa vipi kujiendesha kwa faida wakati kuna makampuni madogo tu ya ndege yalioanza nchini kama mzaha tu,lakini sasa yameanza kutafuta safari nje ya nchi..baada ya kuwa tegemeo lisiloyumba..ktkt safari za nchini..

  Ni aibu kama mtanzania kuamini ati kuendesha shirika la ndege lenye ufanisi ni kazi kubwa sana..mbona kenya na ethiopia mataifa ambayo kiuchumi atutofautiani nayo yamefanikiwa sana kwenye usafiri wa anga??

  siri ya mafanikio yao ni moja kukataa ubabaishaji kama uliokuwepo nchini mwetu

  tatizo kubwa linalotusumbua nchini mwetu ni utamaduni wa kuoneana haya,,baya zaidi tuna utamaduni wa kufuja mali za umma na kusihia kuhamishana kama vile waliofanya wametenda jambo la maana sana hivyo wapewe kitengo kingine wakaangamize.. Kumbe wanatuzamisha kama taifa kama ambayvo leo hii kodi za wananchi badala ya kuetekelezwa kwenye mambo ya maendeleo ya maana ya kuongeza tija na kuchangamsha uchumi wetu zinatumika kulipa mishahara uya wafanyakazi wasiozalisha kabisa

  tunafika wakati sasa kwa serikali kuona mna haki ya kuchoka ingawa ugonjwa mliuleta wenyewe basi dawa mtaitafuta wenye na kuacha mashirika kama atcl na trl na mengine mengi kujiendesha yenyewe kibiashara na yafanye kazi kama mashirika mengine nchini ,,kama ni mitaji serikali ikubali kuweka dhamana ama kuweka reheani mali za trl na atcl ili zijiendeshe zenyewe..hizi n zama za soko huria.. Kila mmoja n lazima apambane ajue jinsi gani ya kuishi kwa jasho lake...utaratibu wa kuendesha kwa kodi za wananchi ausaidii na ni matumizi mabaya ya kodi..na tubadilike sasa..serikali iamue moja kama yanawekeza mtaji yajiendeleze ama yavunjwe kabisa..imefika wakati na wafanyakazi nao wanaitaj haki zao wajue kama shirika lipo ama lah na si kuweka porojo za siasa kila siku

  mh waziri tunaamini siasa za kipuuzi za aliekuwa mh waziri wa miundo mbinu hutozileta tena ofisini mwako....tunaamini mungu atakuongoza na kuwa mwadilifu kushgulikia matatizo ya wizara yako na sio kuweka porojo za siasa
   
Loading...