Utaratibu wa kudai fidia ya bima kwa abiria aliyepata ajali (claim procedure)

muzi

JF-Expert Member
Jun 17, 2016
1,038
1,448
Abiria anapaswa kuandika barua kwenda kampuni husika ya bima iliyokatiwa hilo Bus. Katika barua hiyo aambatanishe vifuatavyo

1.TIKETI YA SAFARI.
2.CHETI CHA MATIBABU YA HOSPITALI.
3. FOMU YA POLISI (PF 3).
4. MCHANGANUO WA GARAMA ALIZOINGIA.
5. PF 90.
6. PF115
7. TIKETI YAKE kama bado anayo (kama imepotea kutokana na mazingira ya ajali itaeleweka haina shida sana).
Cha muhimu ni kwamba kama hakuzidiwa sana basi ahakikishe yeye mwenywe kuwa jina lake lipo kwenye orodha ya majina ya polisi ya majeruhi kwa kutaja majina yake yote kamili.
8. Cheti cha kifo, ikiwa unadai kwa niaba ya ndugu aliyefariki katika ajali.
9. Hakikisha unaziwasilisha nyaraka hizi kwenye ofisi ya bima husika.

KUMBUKA: Utalipwa tu iwapo,ulipanda magari ambayo yaliyoruhusiwa kubeba abiria tu ndiyo (PSV) yaani Passenger Service Vehicles kama vile mabasi ya abiria,daladala, na taxi zilizosajiliwa.

Pamoja na hayo tarajia kupigwa danadana na kuzungushwa sana na wadau husika, cha msingi komaaa kupigania hakiyako. Ulkiona hakuna msaada panda ngazi ya aliyeko juu yake anayekupiga chenga na kukuzunguka. Kumbuka kujenga confidence na kujifanya unajua sheria na haki yako

NB: Kampuni ya bima ikikataa kulipa madai unayoona ni halali, wasilisha mgogoro wako katika ofisi za Msuluhishi wa Migoigoro ya Bima zilizopo PPF Tower Dar es salaam au ofisi ya Mamlaka ya Bima(TIRA) zilizpo nchi nzima

SHARE UJUMBE HUU,ELIMU YA BIMA IWAFIKIE WATU WOTE.
 
Mimi ni mkurugenzi wa Kampuni ya magari ya abiria ambapo gari yetu moja iligongwa na wakati ikibingirika ikasababisha majeruhi kadhaa ndani ya gari na kifo cha mpita njia. Kwa bahati mbaya au makusudi wakati taarifa za polisi zinaandikwa haikuandikwa vyema kama marehemu alipatwa na mauti kama abria au mpita njia ambapo Kampuni ya BIMA imekataa kuilipa familia ya marehemu.

Kwavile fidia imeshindikana kulipwa na BIMA familia imepeleka suala mahakani ambapo kampuni yetu ni mdaiwa. Je ni sahihi kwa Kampuni yetu kushitakiwa? Je katika mazingira kama haya, kampuni yetu inaweza kufanya nini?

Ahsante
 
Sakata kama hilo lina utata, hata kama kesi ikienda mahakamani kinachofuatwa ni kile kilichoandikwa kwenye taarifa ya polisi. Kama hakujumuishwa kwenye Traffic report, maelezo ya polisi ndiyo yatakayokulinda.
Lakini pia ni vizuri kuangalia ubinadamu, zumngumza na polisi watakushauri cha kufanya, ushauri wa polizi ndiyo kielelezo kama utashinda kesi au laah.

Pamoja na yote hayo ni vizuri kukaa na familia husika na kuangalia namna nzuri ya kumaliza swala hilo, maana kuna leo na kesho, na damu ya mtu ikikulilia ni mbaya sana
 
Nashukuru kwa maelezo mazuri sana, nimefuatilia jana kwa kampuni ya BIMA inaonekana familia ya marehemu wameombwa kulipwa kiwango kikubwa zaidi ya Policies za kampuni zinavyosema.Kama ulivyosema kampuni husika nayo iitwe mahakamani THEN huko kila kitu kitajulikana.

Ahsante
 
Back
Top Bottom