UTARATIBU WA KAMPALA INTERNATIONAL UNIVERSITY IN TANZANIA WA KUWAFUKUZA CHUO (DISCO) WANAFUNZI AMBAO HAWAJA KAMILISHA ADA.

melekebu

Member
Sep 30, 2018
7
3
Wakuu poleni na kazi,
nimeshtushwa pale nlipowasiliana na ndugu yangu wa siku nyingi ambaye yeye anasoma chuo cha kimataifa cha kampala baada ya kunipa taarifa kua alichelewa kulipa Ada na ikamgharimu kuingia kwenye chumba cha mtihani bila kukamilisha Ada husika kwa ajili ya kufanya huo mtihani,

Lengo lake lilikua ni kufanya na baada ya wiki mbili kukamilisha iyo pesa, Sasa kaniomba ushahuri sijui afanyeje au aanzie wapi, nimeshan'gaa zaidi pale nlipoona hayo majina yalivyo mengi watu wamepewa suspension na kufutiwa matokeo na wengine discontinue inasikitisha Sana.,,, nimeambatanisha karatasi baadhi ya izo picha.

JE HII NI HAKI? AU KAMPALA INAWAONEA HAWA WATOTO, NAOMBENI MAWAZO YENU.
 
Attachments

  • 20181001_022850.jpeg
    20181001_022850.jpeg
    32.5 KB · Views: 54
  • 20181001_022850.jpeg
    20181001_022850.jpeg
    32.5 KB · Views: 48
  • 20181001_022850.jpeg
    20181001_022850.jpeg
    32.5 KB · Views: 40
  • 20181001_022756.jpeg
    20181001_022756.jpeg
    28.2 KB · Views: 43
Huyo kafoji clearance card itakuwa au kaingia bila kupata ruhusa ya Finance.
 
Sheria ya chuo usipofanya mtihani bila taarifa ni Disco , je ndugu alitoa taarifa kwa uongozi kwamba hawezi kufanya mtihani coz hana ada ? ,kama ali assume , then ajue maisha ya chuo hayana ku-assume ! , haswa pale unaposoma chuo cha private ndio kabisa ,
 
Kuna jamaa alirudishwa akafate Pass ticket ya kufanyia mtihani , tulimshauri amtume mtu alete yani apige simu , yeye aka-assume kwamba kwakua msimamizi anamfahamu atamweleza sababu kwamba amesahau ticket ya kwenda kufanyia paper anapokaa , muda wa mtihani ulipofika msimamizi akamtolea njee kagoma , jamaa ikabidi aulizwe , unafahamu sheria za mitihani hauwezi ingia bila pass ticket , sawa umesahau je haujui kuna taratibu ya ku apply for temporary ticket ? ,so msimamizi ikabidi amwambie akafuate temporary ticket , jamaa akaanza kukimbia kuelekea payment office alipie temporary ticket alipomaliza inabidi isainiwe na teacher wa darasa , then head of department jamaa kumaliza mlolongo wote huo dakika 30 zimeisha sheria hauruhusiwi tena chumba cha mtihani , sasa uzembe kama huo unajitetea vipi na ukumbuke hakuna taarifa hapo , jamaa akapigwa DISCO la nguvu bila kutegemea , maisha ya chuo sio ya ku assume hata kidogo.
 
jamani hivi UDOM unaweza kubadil chaguzi za programme application nyingine
 
Sheria ya chuo usipofanya mtihani bila taarifa ni Disco , je ndugu alitoa taarifa kwa uongozi kwamba hawezi kufanya mtihani coz hana ada ? ,kama ali assume , then ajue maisha ya chuo hayana ku-assume ! , haswa pale unaposoma chuo cha private ndio kabisa ,
Sio kwamba hakufanya mtihani, alifanya mitihani yote husika
 
Kutokulipa ada peke yake sio sababu inayojitosheleza kufukuzwa chuo, ingawa sheria, kanuni na taratibu za chuo( zimeanishwa kwenye prospectus) zinaeleza uwajibikaji wa kulipa ada na kufanya mitihani ni wa lazima.

Kuna uwezekano mkubwa wa fraud & forgery ukichunguza. Mara nyingi kuna jambo nyuma ya jambo ambalo limefanyika mpaka kupelekea huyo jamaa kufukuzwa.

Huenda jamaa alishapewa onyo huko nyuma sisi hatujui, pia labda jamaa ameghushi kibali kinachotoa ruhusa ya kuingia na kufanya mtihani au inawezekana hakuomba ruhusa kwa maandishi kibali cha kuruhusiwa kufanya mtihani au alikataliwa ila alidharau na akafanya paper, kwa hiyo kuna mambo mengi hapo ambayo muhanga hajayaweka wazi.
Ninavyojua vyuo vya binafsi vingi wanafanya sana biashara na hawapo tayari kupoteza kichwa kirahisi kwa kuwa wanajua watapoteza na kukosa pesa pia.

Ushauri wangu kwake jamaa anajua alichofanya yeye mwenyewe atafute njia ya kujishusha na kuomba kufikiriwa arudi chuo( hili linawezekana na ni bora zaidi na halina gharama zaidi ya kulipa deni)
Vinginevyo jamaa atafute mwanasheria kama inawezekana apate ushauri wa kisheria na kufuata hatua za kisheria( njia hii itakuwa na gharama sana pengine kuliko hata ada anayodaiwa).
 
Ni haki kama prospectus itaonyesha kosa la adhabu hiyo

Chuo sio secondary mkuu
Pesa inahitajika ili kuweza kuendesha chuo .
 
Kutokulipa ada peke yake sio sababu inayojitosheleza kufukuzwa chuo, ingawa sheria, kanuni na taratibu za chuo( zimeanishwa kwenye prospectus) zinaeleza uwajibikaji wa kulipa ada na kufanya mitihani ni wa lazima.

Kuna uwezekano mkubwa wa fraud & forgery ukichunguza. Mara nyingi kuna jambo nyuma ya jambo ambalo limefanyika mpaka kupelekea huyo jamaa kufukuzwa.

Huenda jamaa alishapewa onyo huko nyuma sisi hatujui, pia labda jamaa ameghushi kibali kinachotoa ruhusa ya kuingia na kufanya mtihani au inawezekana hakuomba ruhusa kwa maandishi kibali cha kuruhusiwa kufanya mtihani au alikataliwa ila alidharau na akafanya paper, kwa hiyo kuna mambo mengi hapo ambayo muhanga hajayaweka wazi.
Ninavyojua vyuo vya binafsi vingi wanafanya sana biashara na hawapo tayari kupoteza kichwa kirahisi kwa kuwa wanajua watapoteza na kukosa pesa pia.

Ushauri wangu kwake jamaa anajua alichofanya yeye mwenyewe atafute njia ya kujishusha na kuomba kufikiriwa arudi chuo( hili linawezekana na ni bora zaidi na halina gharama zaidi ya kulipa deni)
Vinginevyo jamaa atafute mwanasheria kama inawezekana apate ushauri wa kisheria na kufuata hatua za kisheria( njia hii itakuwa na gharama sana pengine kuliko hata ada anayodaiwa).
Truth!!
 
Abscondment, inawezekana baada ya matokeo yake kuwa NUL amechukuliwa kama hakuonekana kwenye chumba cha mtihani ndio maana akadisco.
Inawezekana pia alikua na Supplementary, kwahiyo baada ya kuwa Null mtihani aliofanya kajikuta anaangukia Supp. Iliwahi kunitokea tena kilikua chuo cha umma, kuna malipo sikufanya na sikujua kama nadaiwa, nimepata Supplementary nikaingia kifua mbele kumnyoosha mwalimu, mwisho wa siku mwalimu akanipigia simu kuwa kuna shida, nilisolve nae nikaandika barua ya kutofanya mtihani ikawa kwenye faili hadi next offered ndo nikapewa chance ya kufanya ile Supp, otherwise ningeachishwa masomo.
 
Back
Top Bottom