Utaratibu upoje katika kutoa Ajira ndani ya halmashauri za miji?

benwise

Member
Oct 24, 2015
98
71
Najua humu jukwani kuna kila aina ya watu toka katika sekta zote, ninaamini hata hili nitajibiwa kikamilifu.

Napenda kujua zile nafasi mbalimbali za vibarua zinazotangazwa na halmashauri za miji mfano kinondoni,tabora nk,hasa vibarua wanaopewa mashine kwa ajili ya ukusanyaji mapato kwenye masoko.

Je, mikataba ya zile ajira ni ya kudumu au muda gani? Na mishahara ni viwango vipi na inalipwaje?Je, mshahara unatoka serikali kuu au ndani ya halmashauri husika?

Naamini wahusika wapo wengi humu naomba watusaidie kutuelewesha vizuri
 
ninachojua ni kwamba, kampuni inapewa kandarasi kwa kazi husika na yenyewe ndio iinaajiri vibarua.
zama za kampuni ziliishaisha mkuu sasa ivi halmashauri zinaajiri wafanyakazi wa muda kwa ajili ya kuusanya mapato zenyewe na mshahara hauvuki 250,000 na haupungui 200,000

enzi za jk ndio tenda zilikua zinapewa kampuni binafsi kama tenda za vyoo, maegesho, masoko na nk ila alivyokuja jiwe wakaona wanaibiwa wakawa wanakusanya wenyewe halmashauri mkuu

utaratibu wa ajira ni kutangazwa na halmashauri na wanafanyisha interview wenyewe sema undugulization ni lazima maana mikataba ni miezi mitatu mitatu hakuna bima ya afyaa, hakuna mafao wala nn na sio ajira za kudumu maana ajira za kudumu wanaoajiri ni public service recruitment secretariate ( psrs) utumishi
 
zama za kampuni ziliishaisha mkuu sasa ivi halmashauri zinaajiri wafanyakazi wa muda kwa ajili ya kuusanya mapato zenyewe na mshahara hauvuki 250,000 na haupungui 200,000

enzi za jk ndio tenda zilikua zinapewa kampuni binafsi kama tenda za vyoo, maegesho, masoko na nk ila alivyokuja jiwe wakaona wanaibiwa wakawa wanakusanya wenyewe halmashauri mkuu
Asante kwa maelekezo mkuu,kwa hiyo mikataba yao inakuwa ni ya muda gani/miezi mingapi?
 
2 Reactions
Reply
Back
Top Bottom