Utaratibu Ukoje Kazini kama mtu anataka kubadili Fani?

fasiliteta

JF-Expert Member
Jul 2, 2014
1,299
2,000
Utajipa stress tu,kubadili siku hizi si Kama zamani mazoea,kwa sasa ajira yoyote mpya inatoka utumishi na ndo mwajiri mkuu.Hao wakurugenzi/Taasisi zq serkali hawana mamlaka hata uwe na PHD lazma ufate taratbu ya kuomba kaxi.

Advantage ni utakua na reference kubwa kwa government.
 

Mnabuduhe

JF-Expert Member
May 8, 2015
323
500
Wakuu naomba kujua mfano mtu ameajiliwa na Diploma ya Mechanical engineering au Electrical engineering Serikali baada ya kufanya kazi kwa miaka kadhaaa ameamua kutaka kujiendeleza lakini sio katika hio fani aliyo ajiliwa nayo badala yake anataka kwenda upande wa Account au IT yani achukue degree nyingine kabisa hapo imeeakaje kuhusu ruhusu na promotion baada ya ku graduate?

Kubadili Kazi! Ni utaratibu wa Kawaida hasa kwenye Taasisi ambazo zinahitaji watu wa fani unayotaka kuisomea.
Unapoamua Kusomea Kitu kingine hakikisha unajua Faida na Hasara utakazoweza kuzipata pindi utakafanyiwa recategorization.
Ulikuwa ni technician wa mechanics utakaposomea Fani ya IT utafanyiwa RECATEGORIZATION na HR kuwa IT Tech. kulingana na ngazi ya elimu uliyosomea; Diloma au Bachelor.

Unapofanyiwa Hiyo kitu unaweza usipoteze au ukapoteza maslahi fulani.
Unapofanyiwa Recategorization na ukakuta ulishapanda daraja hata moja;mfano Ulianza kazi na Diploma ya Mechanics ukaanzia daraja C - la Mshahara na ukapanda kwenda daraja D - Utakapofanyiwa Rec, utapaswa kurudi na kuanzia Daraja la Mshahara wa Fani uliyosomea (ENTRY POINT)- Kama Dipl - Utaanza na C, na iwapo ni bachelor utaanza na D.

Jaribu kuomba Ushauri mahususi juu ya fani unayotaka kusomea! Hasa kwa Wakongwe Kazini, Usije ukasoma Fani ambayo Mwajiri wako Haiitaji watu wa elimu yako.

Epuka Kuomba Msaada kwa Kila Mtu! Wengine wanaweza wasifurahi wakakukatisha Tamaa.
Kama Unamwamini Mwajiri wako na Unajua ni Mtu Mwema na Mkweli waweza mfuata na Kumshirikisha.

Kila la Heri.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom