Utaratibu Kuhusu Kustaafu kwa hiari kwa watumishi wa Umma

CHIBA One

JF-Expert Member
Nov 16, 2018
560
2,087
Sheria ya utumishi wa Umma inasemaje kwa mtumishi ambaye anataka kustaafu kwa hiari kabla ya miaka ile 60 ya kisheria..

Mfano ana miaka 55. ila kwa sababu ya changamoto ya ugonjwa anaamua kustaafu kwa hiari..

Je anatakiwa kufata taratibu gani?

Katika kipindi ambacho anasubiri mafao ataendelea kupokea mshahara?

Nna ndugu Yangu ana hii changamoto wakuu na haoni tena kama ataendelea kufanya kazi kwa changamoto yake.
 
Kustaafu kwa hiari ni unapofikisha 55, unaandika tu barua kwa mwajiri wako na kuelezea sababu zako. Mwajiri akiridhia anakupa barua. Hulipwi mshahara wakati unasubiria mafao, si umeshastaafu, unalipwa nn tena
 
Kustaafu kwa hiari ni unapofikisha 55, unaandika tu barua kwa mwajiri wako na kuelezea sababu zako. Mwajiri akiridhia anakupa barua. Hulipwi mshahara wakati unasubiria mafao, si umeshastaafu, unalipwa nn tena
Oooooh okay Mkuu,
 
Unatakiwa utoe notification kwa mwajiri wako miezi sita kabla ya tarehe unayotarajia kustaafu kwa hiari. Kustaafu kwa hiar iko kisheria kwahiyo mwajiri hana mandate ya kukukataza, hata isipokuwa kwa tatizo la ugonjwa una uwezo wa kustaafu kwa hiari. Mwajiri atakuandikia kibali cha kustaafu ambacho utakipeleka ofisi za psssf na wao watakupa fomu yenye maelezo ya kujaza na vitu unavyotakiwa kuviwasilisha kwao ili wakuandalie mafao yako ya kustaafu. Ushaur wangu ukipeleka vitu vyako psssf uende na dispatch uwasainishe kukubali kupokea kwan wana tabia ya kupoteza document za watu na kukana kuwa uliwasilisha. Swala la kuendelea kupokea mshahara hauwez kuendelea kupokea kwan utakuwa umeshastaafu
 
Back
Top Bottom