Utapeli/Wizi Madukani; Nimetapeliwa 744,000, Nifanyeje?

Ellies

New Member
Jun 23, 2015
1
2
Wadau, mimi nina duka la jumla na rejareja.

Jana walikuja jamaa watatu na gari ndogo nyeupe aina ya Mark II, ''Plate Number nimehifadhi''. Wakanunua bidhaa za jumla ya kama 945,000/- na kumlipa kijana kabla ya kupakia mzigo. Kijana alizihesabu na kuhakiksha zimetimia kabisa kisha kuzihifadhi sehemu iliyofungwa. Wakaendelea kupakia mizigo, hatimaye wakamaliza. Baada hapo wakaanza kuondoka, kijana akawaomba mawasiliano kama wateja wazuri ila wakakataa kabisa kabisa. Punde alivyorudi kucheki zile pesa ghafla akakuta zimepungua sana, kabla ya kuhakiki ni kiasi gani ndipo akakimbia kunakili namba za gari. Wakati huo anadai alikuwa na kizungu zungu. Sasa baada ya kutulia, katika hesabu akakuta imebaki 201,000/- pekee. Yaani 744,000/- ilikuwa imepotea katika mazingira hayo ya kutatanisha.

Wadau naomba ushauri, je nifanye nini? Kuna aliyewahi kupitia au kusikia jambo kama hili?
 
Mazinga umbwe mkuu, watu na fani zao(ila za mwizi ni 40 watanaswa tuu)
 
Kuna dogo wa M-pesa majuzi pale kunduchi wanapaita mtongani nilienda kutoa sent kwa dogo anaitwa JOSE,,, mara kaja mzee wa Heshima kuweka laki nane,ile anaondoka,,dogo kucheki mkononi kabakia na elfu mbilimbili za thamani ya laki na sitini,,,bahat nzuri yule taperi alikuja na bajaj,,dogo akawai kuchukua bodaboda kumfukuzia,wakamkamata,,akawataja wenzie anaoshirikiana nao SIJUI wanaitwa kina Beng'a ,,ilibidi awapigie wenzie wakatuma million,,wazee Wakala laki mbili,, na zile elfu mbilimbili dogo aliogopa Kukaanazo,,wazee wakamuambia kazilete tuziifadhi hapa kituoni
 
Wadau, mimi nina duka la jumla na rejareja.

Jana walikuja jamaa watatu na gari ndogo nyeupe aina ya Mark II, ''Plate Number nimehifadhi''. Wakanunua bidhaa za jumla ya kama 945,000/- na kumlipa kijana kabla ya kupakia mzigo. Kijana alizihesabu na kuhakiksha zimetimia kabisa kisha kuzihifadhi sehemu iliyofungwa. Wakaendelea kupakia mizigo, hatimaye wakamaliza. Baada hapo wakaanza kuondoka, kijana akawaomba mawasiliano kama wateja wazuri ila wakakataa kabisa kabisa. Punde alivyorudi kucheki zile pesa ghafla akakuta zimepungua sana, kabla ya kuhakiki ni kiasi gani ndipo akakimbia kunakili namba za gari. Wakati huo anadai alikuwa na kizungu zungu. Sasa baada ya kutulia, katika hesabu akakuta imebaki 201,000/- pekee. Yaani 744,000/- ilikuwa imepotea katika mazingira hayo ya kutatanisha.

Wadau naomba ushauri, je nifanye nini? Kuna aliyewahi kupitia au kusikia jambo kama hili?
Ila nawe jiulize ilikuwaje dogo arudi kuhesabu hela ghafla baada ya wateja kuondoka? Kama alishajiridhisha kwamba hela ilikuwa sahihi nini kilimlazimisha kurudia kuhesabu, wakati mwingine kijana anaweza kufanya dili akatengeneza mazingira ya kukuaminisha uchawi, fikiri zaidi ndugu
 
Kuna mwingine huku nanjirinji kalizwa milioni na laki mbili, jamaa walijifanya wanasajili line za halotel wakamwambia muuza duka kuwa simu yao imezima wanaomba kutumia simu yake, hilo ni kosa wakahamiha salio la aitel money kwenda kwenye simu yao, jamaa walikamatiwa NAKAPANYA walikodi NOAH walikuwa wanatorokea TUNDURU
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom