Utapeli wastukiwa katika usajili wa gazeti la Lete Mambo

NI MTAZAMO TU

JF-Expert Member
Feb 20, 2014
1,203
998
Idara ya Habari (MAELEZO) imebaini nyaraka za kughushi zilizowasilishwa na Mmiliki wa Kampuni ya FUKANI, Joseph Sheka wakati alipoziwasilisha kwa ajili ya kusajili gazeti la LETE MAMBO.

Akizungumza na waandishi wa habari jana Jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi wa MAELEZO, Dkt. Hassan Abbasi alisema kuwa mtuhumiwa huyo aliwasilisha nyaraka mbalimbali akidai kuwa ni za Mamlaka ya Mapato (TRA) ambazo uchunguzi wa awali umebaini kuwa mihuri na sahihi za baadhi ya maafisa wa Mamlaka hiyo zilizotumiwa ni za kughushi.

“Ni vyema jamii ikafahamu kuwa huu siyo wakati wa kujaribu kuishi kwa njia zisizo halali, kila mwananchi anapaswa kufuata taratibu zinatohitajika pindi anapotaka kupatiwa huduma katika maeneo mbalimbali ya ofisi za Umma."

Dkt. Abbasi alitoa rai kwa ofisi mbalimbali za Umma kuwa makini na nyaraka zinazowasilishwa na wateja wao kwani zinaweza kuwa na malengo mbalimbali ya kuiingiza Serikali katika matatizo hivyo kuitia hasara.

Mbali na hayo Dkt abbasi alisisitiza kuwa wale wanaohisi waliwasilisha nyaraka zao na kuona kwamba zina utata kuja kuzirekebisha na watakaobainika kuwa walighushi nyaraka hizo sheria itafuata mkondo wake.

Kwa sasa Idara ya Habari imemkabidhi mtuhumiwa katika Kituo cha Polisi cha Kati jijini dar es salaam kwa mahojiano zaidi.
 
Hii sasa basi, watu wamezidi mno kuwa wasanii, kwanini ughushi taarifa zako kama unafanya mambo yako au kazi zako kihalali?

Naungana na Msemaji aliyesisitiza ".........wale wanaohisi waliwasilisha nyaraka zao na kuona kwamba zina utata kuja kuzirekebisha na watakaobainika kuwa walighushi nyaraka hizo sheria itafuata mkondo wake". Ni vema Watanzania tukajiuliza tumelifanyia nini taifa linalohusu maendeleo?
 
Utapeli wastukiwa katika usajili wa gazeti la Lete Mambo......Mmiliki Atupwa Selo

Idara ya Habari (MAELEZO) imebaini nyaraka za kughushi zilizowasilishwa na Mmiliki wa Kampuni ya FUKANI, Joseph Sheka wakati alipoziwasilisha kwa ajili ya kusajili gazeti la LETE MAMBO.

Hii sasa basi, watu wamezidi mno kuwa wasanii, kwanini ughushi taarifa zako kama unafanya mambo yako au kazi zako kihalali?

Naungana na Msemaji aliyesisitiza ".........wale wanaohisi waliwasilisha nyaraka zao na kuona kwamba zina utata kuja kuzirekebisha na watakaobainika kuwa walighushi nyaraka hizo sheria itafuata mkondo wake". Ni vema Watanzania tukajiuliza tumelifanyia nini taifa linalohusu maendeleo?
Sasa hapo ikija kufuatiliwa hilo tatizo ni kubwa sana hasa kwenye usajili wa makampuni au taasisi nyingine.
Muhimu lifamyiwe kazi
 
Idara ya Habari Maelezo leo memkabidhi kwa Polisi Dar es Salaam, ndugu Joseph Sheka baada ya kubaini kuwa alitaka kusajili Gazeti kwa kutumia nyaraka feki za Mamlaka ya Mapato Tanzania(TRA).

C14tVLUXcAIPLXu.jpg

C14tZOGXEAA-nmb.jpg
 
2 Reactions
Reply
Back
Top Bottom