Utapeli wa nyumba unaoshika kasi Mbagala Chamazi na Chanika

Nafikiri sio utapeli maana unapata mali according to your money, kama unataka cement itoe matofali 18 utalipa milioni 100, hao jamaa acha wahudumie hiyo market ya watu wa chini kuna watu wanahitaji na ndio wanapoweza, usitake Mercedes Benz kwa bei ya Toyota
Bila shaka nawe mjenzi wa nyumba uchwara
 
Kwani umeshauza ngapi
Sio nimeuza ngapi!!!?....umedanganya umma wa Watanzania! Unadhani serikali yako haioni ubora wa zile nyumba? Unafikiri wote wanaonunua zile nyumba ni Wajinga? Unadhani wanajenga bila vibali vya ujenzi? Na nikuhakikishie tu ndugu Nyumba hizi unazosema hazina ubora na hazina lenta na baadhi ya kuta hizo ni Uongo kabisa! Nyumba ni nzuri na zinauzika freshi tu tatizo mkishaanza kumiliki hizi smartphone mnakuwa waandishi wa Habari!
 
Sio nimeuza ngapi!!!?....umedanganya umma wa Watanzania! Unadhani serikali yako haioni ubora wa zile nyumba? Unafikiri wote wanaonunua zile nyumba ni Wajinga? Unadhani wanajenga bila vibali vya ujenzi? Na nikuhakikishie tu ndugu Nyumba hizi unazosema hazina ubora na hazina lenta na baadhi ya kuta hizo ni Uongo kabisa! Nyumba ni nzuri na zinauzika freshi tu tatizo mkishaanza kumiliki hizi smartphone mnakuwa waandishi wa Habari!
Ndugu Kicheche Mkali bila shaka mwenyewe ni jenga uza au dalali wa jenga uza ndio maana watetea ugali wenu.Vibali hailalishi ubora wa nyumba hiyo inayo jengwa ,iliyojengwa.Kwani hata utaratibu wa ukaguzi wa ubora haupo kwa sasa.Kipimo pekee ni vilio vya wauziwa nyumba zenyewe.Kwani hata Mashimo ya choo,jenga uza hachelewi kumuwekea chini ya sebule,urefu wenyewe akibahatika futi tano🤔
 
Ndugu Kicheche Mkali bila shaka mwenyewe ni jenga uza au dalali wa jenga uza ndio maana watetea ugali wenu.Vibali hailalishi ubora wa nyumba hiyo inayo jengwa ,iliyojengwa.Kwani hata utaratibu wa ukaguzi wa ubora haupo kwa sasa.Kipimo pekee ni vilio vya wauziwa nyumba zenyewe.Kwani hata Mashimo ya choo,jenga uza hachelewi kumuwekea chini ya sebule,urefu wenyewe akibahatika futi tano
Hii sio kweli budah....
 
Kuna wimbi la nyumba nzuri na za kisasa kwa mwonekano zinaziuzwa kwa bei chee 25m-45m Mbagala Chamazi na Chanika jijiji DSM.

Mchezo upo hivi:

Kuna jamaa wana viwanja vingi na wana mafundi wao ambao hujenga nyumba cha kiwango cha chini sana cement mfuko mmoja tofali 48+ tofali hufwatuliwa site na kujenga hapo hapo.

Bati gauge 32 wanapiga rangi wenyewe. Baadhi ya kuta wameweka play wood badala ya tofali kitaalam sana.

Kench zipo mbali mbali sana kubana matumizi ya mbao. Ndo maana nyumba zote laizma ziwe na gypsum kuficha mambo.
Nyumba huwa hazijakaliwa na watu means bado mpya.

Hazina lenta ndo maan lazima wapige plasta na kuweka gypsum kuficha. Kuna wataalam wa kuchanganya rangi ili kukubabaisha uingie kingi. Msingi tofali moja tu ishapanda

NB: Nyumba hizi hazichukui muda sana utaona nyufa balaa. Na walengwa wengi ni wastaafu ambao hutafuta nyumba za kuishi baada ya kustaafu.
labda wamejengewa wasitaafu kutokana na life span yao
 
Halafu eti tuna "taasisi/mifuko ya wastaafu" inafanya kazi gani ilhali walengwa wao wanakuwa na maisha ya hovyo wakistaafu!!??
Kumuhifadhia mtu tu pesa zake sio lengo kuu la kuanzishwa kwa hiyo mifuko,bali ni kuhakikisha maisha yao baada ya kustaafu yanakuwa mazuri na salama.
Wastaafu wanapata tabu sana wametumikia nchi kwa jasho na damu, wanatapeliwa na Qnet, Mr. Kuku, DECI, AIM Global na sasa hivi kwenye nyumba
 
Hapo Dawa ya hili suala lipo kwenye Mikataba.
Sheria ya mauziano ya nyumba zipo, ambapo Serikali inatakiwa ishirikishwe na kodi ya TRA kulipwa.
-Sheria imetaja wazi haki za manunuzi na za muuzaji.
-Lazima muwekeane kipengele cha gurantee.
 
26 Reactions
Reply
Back
Top Bottom