Utapeli wa kwenye simu kujifanya Wakala wa Tatu Mzuka! TCRA mpo wapi?

Domhome

JF-Expert Member
Jun 28, 2010
2,834
2,000
WALINITUMIA SMS HIZI:-
24 Feb 2019 SAA 2305
+255 745 995 827 alituma SMS hii:

Tatu Mzuka (JACKPOT) Hongera Umeshinda TSh.6,000,000/=milioni Sita Katika Droo Ya Saa 11 . Tatu Mzuka Inabadilisha Maisha Yako Kamp No 555111 Tupigie Simu. No, 0768146006.


26 Feb 2019 SAA 2158
+255 768 146 006 alituma SMS hii:

Tatu Mzuka (JACKPOT) Hongera Umeshinda TSh.6,000,000/=milioni Sita Katika Droo Ya Saa 11 . Tatu Mzuka Inabadilisha Maisha Yako Kamp No 555111 Tupigie Simu. No, 0765669354.

Hao jamaa hapo juu yaani +255 745 995 827 (Megi Simtengu) na +255 768 146 006 (Silon Adam) wakishirikiana na +255 765 669 354 (Safia Hamisi) walijaribu kunitapeli kwa nyakati mbili tofauti kama SMS zinavyojionyesha hapo juu...

Mara ya kwanza (24 Feb 2019) niliamua kukaa kimya ili kuwapotezea lakini wakaamua kurudia tena Jana (26 Feb 2019) na nikaona ni heri niwaweke wazi hapa JF ili members wawe makini na wahuni hawa....

Polisi na TCRA Nina imani mmo humu jamvini tafadhalini wafatilieni wahuni na wezi hawa wa mtandao. Kwangu wamenoa lakini inawezekana wengine wakaingizwa mkenge na watu hawa....

Domhome,
27 Feb 2019

Sent using Jamii Forums mobile app
 

Adrian Stepp

Verified Member
Jul 1, 2011
2,445
2,000
Kwanini usitumie proper channels ku-address hoja zako? Sidhani kama humu itasaidia anyway!
 

Uta Uta

JF-Expert Member
Feb 2, 2016
3,469
2,000
Mi walinipigia wakaniambia wanataka kunipa biashara nisimamie, mi nikamwambia sina uzoefu na biashara hivyo anipe mata ko hayo naweza kuyasimamia vizuri. Haaa jama lilinitukana na kukata simu yaani mi huwa nawajibu shombo na hawa ni watu wa karibu sana mi nna laini za mitandao mitatu na nilitumia sms na mtu mmoja laini zote 3
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom