Singida ndio home
JF-Expert Member
- Feb 23, 2012
- 3,192
- 3,353
Ni kijana ambae hapo nyuma amepata kufanikiwa kwa haraka sana na kuishi maisha ya juu sana na kukiri kuwa na uwezo wa kutengengeneza takribani milioni 9 kila wiki, Ilifikia kipindi akanunua gari ya kifahari aina ya BMW X6, sijui kama ilikuwa ni bahati mbaya au maksudi kimaslahi hio gari ilikula mzinga wiki kama sio miezi michache kabla hajaondoka nchini ikiambatanishwa na "tetesi" ya kwamba kuna aina za bima endapo gari ikipata ajali shirika la bima humlipa mmiliki pesa taslim ya kununua gari upya.
Kijana kwa sasa hayupo nchini na inadaiwa anatafutwa na polisi kwa kile kinachosadikiwa ya kwamba kakimbia na pesa anazodaiwa na wawekezaji wake waliowekeza pesa zao kwake ili wapate faida kwa kuziongeza kupitia skills za forex alizonazo kijana. Kuna "tetesi" ya kwamba wawekezaji walioowekeza wanamdai kiasi cha dola laki tatu (takribani milioni 690 za kitanzania).
HITIMISHO
Walengwa wanaomdai huyu kijana inawezekana wakadhani kwamba kijana kakimbia na pesa zaokumbe sivyo , Kijana kaahidi ya kupitia account yake ya twiiter kwamba atarudisha pesa zao, walengwa itapendeza wawe wavumilivu wakiwa na uhakika wa kurejeshewa pesa zao.
NJE YA MAADA
Awali majuzi tarehe 7 - 5 -2019 huko nchini afrika kusini mfanya biashara wa forex aliekuwa na pesa chafu ambae pia wawekezaji walikuwa wakiwekeza pesa kwake kwa jina la "jabulani cashflow ngcobo" amefungwa kifungo cha miaka sita na kulipa faini ndefu baada ya kupatikana na kesi ya kutapeli wawekezaji
CHIMBUKO LA FOREX TANZANIA
Miaka ya 2017 kuna kijana anaefahamika kwa jina la "Ontario a.k.a Sir jeff dennis" ndie aliekuwa chanzo cha watanzania wengi kuanza kuisoma, kuifatilia na kuifanya forex, alileta muamko mkubwa sana wa forex nchini ikafika kipindi habari ya mujini ilikuwa ni forex na hata post yake ilivunja rekodi ya ushawishi mkubwa kwenye mtandao wa jamiiforums kwa kuwa na wasomaji wengi. Baada ya miezi michache kijana huyu alianzishiwa maada / thread kibao humu ndani zilizomshtumu kwamba ni mpigaji aliekuwa analazimisha wanafunzi wake watrade kwa kumtumia broker waliekuwa wanagawana faida