Utapeli wa ccm kwa mwananchi wa yombo dovyo mpaka buzza | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Utapeli wa ccm kwa mwananchi wa yombo dovyo mpaka buzza

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by NewGeneration, Nov 24, 2009.

 1. NewGeneration

  NewGeneration Member

  #1
  Nov 24, 2009
  Joined: Aug 8, 2009
  Messages: 6
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hivi ndivyo wakazi wanaotumia barabara ya kuanzia devis corner kuelekea vituka na buza walivyo tapeliwa na baadhi ya viongozi ambao walikuwa wanagombani uongozi wa serikali za mitaa kupitia chama cha mapinduzi (ccm). Wakati wakampeni ndogo hizo zilizofanyika mwishoni kwa mwezi uliopita, agenda kuu ambayo ilikuwa ikizungumziwa na wagombea hao wa ccm walikuwa wakidai kuwa barabara hiyo ilishapata mkandarasi wa kuitengeneza kiwango cha lami, ili wakuweza kuwapata vizuri wakazi hao. Ghafla tu, tuliona bango kubwa la kuashiria barabara itaanza kujengwa tena bango lenyewe waliliweka siku ile ile ya uchaguzi yaani tarehe 25/10.

  Lakini baada ya mimi kufanikiwa kulisogelea lile bango na kulisoma vizuri nilishangazwa kuliona hilo bango kukosa baadhi ya taarifa muhimu ambazo zinaonyesha kuwa kuna ukweli wa hii barabara kutengezwa. Kama unavyo weza kujionea contractor ambaye ametajwa hapo hakuandikiwa address yake, wala hakuna consultant aliyetajwa. huu kama sio utapeli nini jamani? Eti wa jamii forums, ebu nielewesheni hivi ndivyo mabango yote ya ujenzi wa barabara yanavyo andikwa.

  tutaendelea kudanganyika hadi lini? Barabara sasa ni mbovu kupita maelezo.

  Picha imechukuliwa kwa simu, samahani kama itakuwavigumu kuiona vizuri. Ila unaweza ukaidownload than ukai zoom vizuri zaidi.
   

  Attached Files:

 2. Shedafa

  Shedafa JF-Expert Member

  #2
  Nov 24, 2009
  Joined: May 21, 2008
  Messages: 802
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 35
  Kumbe siye peke yangu niliyeshangazwa na kiini macho cha hii barabara!, zaidi ya hapo nyumba kibao zimetiwa alama kama zinataka kubomolewa maana zimo ndani ya barabara lakini imekuwa kwa ghafla tu. Jinsi ya mchakato wa kubomolea watu nyumba kwa ajili ya upanuzi wa barabara unavyokuwa na kasheshe leo hii eneo hili la hii barabara limekuwa rahisi hivi, ngoja tuone. Kingine yale maeneo korofi hatujasikia hatima yake, kwa mfano ule mteremko wa kwa Jimmy siku nyingi watu wametangaziwa kubomolewa na wamekuwa wakisubiri kinachoendelea lakini imekuwa kimyaa.
  Kama kweli ilikuwa ni ujanja wa uchaguzi basi wajue kuna mwingine mwakani, waanze kutafuta uongo mwingine.
   
 3. Lunyungu

  Lunyungu JF-Expert Member

  #3
  Nov 24, 2009
  Joined: Aug 7, 2006
  Messages: 8,836
  Likes Received: 75
  Trophy Points: 145
  CCM hakika sijui inakuwaje hata wanashinda kura kibao na mitaa kibao Dar ambako watu wanaijua kwa uovu wake lakini mikoani ambao wanaitegemea Dar wanaikataa CCM .Acha watu wawekwe sawa waelewe CCM ina matapeli .
   
 4. Geza Ulole

  Geza Ulole JF-Expert Member

  #4
  Nov 24, 2009
  Joined: Oct 31, 2009
  Messages: 11,047
  Likes Received: 3,954
  Trophy Points: 280
  Lakini Watanzania tuache upuuzi Yombo vituka yote ilipimwa hiyo barabara imekwama kwavile watu walijenga barabarani hasa Machimbo na hata bonde la kwa Jimmy sehemu zote hizo zilishapimwa toka kipindi cha watu wa Kurasini walipoamishwa na Watu wa Malawi walipokuwa wanajenga oil storage facilities Kurasini! hao watu hawastahili kulipwa kisheria! Ndo maana hatuendelea nchi hii ufisadi mpk kwa wananchi
   
 5. Dr. Chapa Kiuno

  Dr. Chapa Kiuno JF-Expert Member

  #5
  Nov 26, 2009
  Joined: Sep 11, 2009
  Messages: 445
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Kwa kweli hawa watu wanatuuza tu! Ss sera mpya inakuja ambayo ni VIJANA kupata Vyeo vya juu kuanzia mwakani! Mhh....
   
 6. Mbonea

  Mbonea JF-Expert Member

  #6
  Nov 30, 2009
  Joined: Jul 14, 2009
  Messages: 640
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Ha ha haaaa! Siasa tamu kweli
   
Loading...