mama D
JF-Expert Member
- Nov 22, 2010
- 19,760
- 35,205
Watu hawakomagi jamani😎😎😎Naomba watanzania muwe makini sana na kijana anaitwa Peter Kasanga aliyeko mkoani mwanza mwenye kampuni ya fx fire, anafanya biashara ya uwekezaji yaani unawekeza pesa na mwisho wa mwezi unalipwa 60% ya kiasi cha pesa ulicho wekeza, alikuwa akifanya hii biashara ya uewekezaji tangu mwaka jana mwanzoni, alikusanya pesa za watu zaidi ya 300, huu ni mwezi wa 5 ajatoa pesa kwa wawekezaji waliowekeza.
Cha kushangaza anazidi kupokea pesa kwa wawekezaji wapya wakati ajalipa pesa kwa wawekezaji wa muda mrefu ajawalipa huu mwezi wa 5, naomba watanzania ambao mtakutana na matangazo ya uwekezaji toka kampuni inaitwa fx fire ambayo mmiliki ni peter kasanga mwenye namba hizi za simu 0744951631, 0626215507, 0742725683 bado anaendela kukusanya pesa za watu kwa kuwa akikishia kuwa baada mwezi watapokea 60%, mwezi ukifika anatoka visingizio kuwa pesa zimefungiwa benki.
Naomba mkuu wa takukuru mkoa wa mwanza, OCD mkoa wa mwanza, DSO na RSO fikeni jengo la Rock City Mall iliyopo ofisi ya fx fire muone namna ya kuwasaidia watanzania ambao wametapeliwa na huyu peter kasanga