Utapeli wa biashara ya kuwekeza unaofanywa na kampuni ya FX Fire iliyopo mkoani Mwanza

kibwengo2020

New Member
Nov 6, 2018
2
5
Naomba watanzania muwe makini sana na kijana anaitwa Peter Kasanga aliyeko mkoani mwanza mwenye kampuni ya fx fire, anafanya biashara ya uwekezaji yaani unawekeza pesa na mwisho wa mwezi unalipwa 60% ya kiasi cha pesa ulicho wekeza, alikuwa akifanya hii biashara ya uewekezaji tangu mwaka jana mwanzoni, alikusanya pesa za watu zaidi ya 300, huu ni mwezi wa 5 ajatoa pesa kwa wawekezaji waliowekeza.

Cha kushangaza anazidi kupokea pesa kwa wawekezaji wapya wakati ajalipa pesa kwa wawekezaji wa muda mrefu ajawalipa huu mwezi wa 5, naomba watanzania ambao mtakutana na matangazo ya uwekezaji toka kampuni inaitwa fx fire ambayo mmiliki ni peter kasanga mwenye namba hizi za simu 0744951631, 0626215507, 0742725683 bado anaendela kukusanya pesa za watu kwa kuwa akikishia kuwa baada mwezi watapokea 60%, mwezi ukifika anatoka visingizio kuwa pesa zimefungiwa benki.

Naomba mkuu wa takukuru mkoa wa mwanza, OCD mkoa wa mwanza, DSO na RSO fikeni jengo la Rock City Mall iliyopo ofisi ya fx fire muone namna ya kuwasaidia Watanzania ambao wametapeliwa na huyu Peter Kasanga.
 
Yani uweke pesa yako yeye akupe faida ya 60% huoni kama kila anayejiunga upeo wake wa kufikiri ulikwama hapo...acheni shortcut...huyo ni tapeli
 
Duh poleni wahanga! Ila jamani bado tu hamshtuki na hizi biashara! Mtu anakuahidi kukupa 60% kwa biashara gani hasa hushtuki mtu kukushikia pesa yako?🤷‍♂️ hizi shortcuts zinatukucost.
Watu wana vichwa vigumu, yani eti mtu anakupa uhakika wa kupata faida.
 
Huyo jamaa namfahamu aliacha chuo sahivi angekuwa 3rd year UDOM, sijui kwanini aliamua kufungua ofisi Mwanza kwenye Plaza gani ile kubwa zaidi nimesahau jina.

Money management ndio itakuwa ilimshinda. Alichukua hela mwanzoni akawa anarudisha na ushahidi juu baadae akaanza kuchelewa, baadae wanachuo wakaacha kumpa hela zao, akabaki na raia wa mtaani. Ndio maana hata usajiri wa kampuni yake ulicheleweshwa na mamlaka za Mwanza kwa wasiwasi wa utapeli.

Hapo ukute alichoma akakosa hela ya marejesho akaona akusanye zaidi ili hela inayoingia afanye trading kisha alipe malipo ya awali. Kama sio mwizi mkikaa mkatulia hela yake mnapata, endapo itapatikana. Kwake yeye na wengine wakomavu kuweka 1M na kupata 2M kwa wiki ni kawaida.
 
Tafuteni elimu kwanza kisha m trade wenyewe. Utampaje mtu hela yako akusaidie ku trade? acheni uvivu bhana.
 
Hivi hao mnaowaita matapeli na mpaka namba zao za simu mnaziweka humu kwa nini hamuwaripoti mahali husika ama hamtaki kumfaidisha DPP ambae amekuwa ndio mnufaika mkuu wa pesaza wapenda vitonga
 
Naomba watanzania muwe makini sana na kijana anaitwa Peter Kasanga aliyeko mkoani mwanza mwenye kampuni ya fx fire, anafanya biashara ya uwekezaji yaani unawekeza pesa na mwisho wa mwezi unalipwa 60% ya kiasi cha pesa ulicho wekeza, alikuwa akifanya hii biashara ya uewekezaji tangu mwaka jana mwanzoni, alikusanya pesa za watu zaidi ya 300, huu ni mwezi wa 5 ajatoa pesa kwa wawekezaji waliowekeza.

Cha kushangaza anazidi kupokea pesa kwa wawekezaji wapya wakati ajalipa pesa kwa wawekezaji wa muda mrefu ajawalipa huu mwezi wa 5, naomba watanzania ambao mtakutana na matangazo ya uwekezaji toka kampuni inaitwa fx fire ambayo mmiliki ni peter kasanga mwenye namba hizi za simu 0744951631, 0626215507, 0742725683 bado anaendela kukusanya pesa za watu kwa kuwa akikishia kuwa baada mwezi watapokea 60%, mwezi ukifika anatoka visingizio kuwa pesa zimefungiwa benki.

Naomba mkuu wa takukuru mkoa wa mwanza, OCD mkoa wa mwanza, DSO na RSO fikeni jengo la Rock City Mall iliyopo ofisi ya fx fire muone namna ya kuwasaidia watanzania ambao wametapeliwa na huyu peter kasanga
Mbona hapokei jaman... Nina ka hela kangu nataka niwekeze hapo
 
Hivi kumbe hela huwa zipo sana eeeh ivii unakubali vipi kutoa hela yako na kumpa mtu atrade then utapata 60% ... tuweni makini jaman alafu na wewe ulietoa taarifa humu ungetafuta mamlaka husika kama kwel unauchungu na wananchi sisi hizo namba hazitusaidiii chochote.
 
Back
Top Bottom