seifutz
Member
- Jul 18, 2021
- 34
- 113
Mimi Naishi Dar es salaam, Nina Mdogo watu Yupo Dodoma Mpwapwa.
Juzi Mwezi Huu wa 09 / 2021 alipigiwa Simu na Mtu anaemfahamu kabisa.
Akamwambia Kuna Ajira imepatikana kwake na Angetoka kimaisha kwa Kufanya hiyo kazi.
Jamaa Akamueleza Kuwa Asafiri Kwenda Kigoma ili akampe huyo mchongo,
Sasa kwa kuwa Dogo Alikuwa anamfahamu Jamaa kwa hiyo hakuweka wazo la kuwa hiyo ni sehemu ya hatari.
Basi Bana Kutokana na Ushawishi Aliyoyfanya huyo Jamaa ikabidi Dogo Anipigie Simu kuwa kapata Kazi Kigoma.
Dogo ni Mpambanaji sana sikutaka kumzuia ila nilimpa Tadhari tu awe makini.
Kwa Nauli Yake Akasafiri Akiwa amejipanga Hadi mahitaji yake ya msingi kama Unga mafuta na pesa ya matumizi sababu aliambiwa utakuwa unajitegemea.
Akafika kigoma, Baada ya hapo akapelekwa Kwenye Semina.
Kwa kuwa wale watu yeye hawafahamu alikaaa kwenye semina yao siku 1 na hapo akaambiwa atoe 20000 kwa Ajiri ya form ya kujiunga akatoa.
Kwenye Sehemu alipostuka ni pale Alipoambiwa Anatakiwa Kutoa Laki 6 ili kuingizwa kwenye Mfumo kama Mwana Chama Sasa na hapo atakuwa anapata pesa kutokana na Watu atakaokuwa anawaleta kujiunga.
Dogo akanipigia Simu , mm nawafahamu hawa watu nikamwambia Hapo Hakuna Kazi Dogo Rudi Tu.
Sasa alipokuja kuonyesha msimamo wake kuwa hayupo Tayari na anataka kurudi ndipo matatizo yalipo Anza.
Kwanza Alienda Kuoga Kurudi akakuta wamepangua begi lake na kuchukua 10000,
Pesa Ya akiba aliyokuwa nayo ni 80000, Baada ya kuchukua 10000 akabaki na 70000,
Mm nikamwambia hiyo pesa iliyobaki aweke kwenye Simu hadi atakapokuwa anataka kusafiiri.
Sasa hadi ninapoandika huu ujumbe Dogo kwanza kuna muda hapatikani na akipatikana simu haipokelewi.
Na sio Kawaida yake.