Rais Wa Malofa
JF-Expert Member
- Aug 27, 2015
- 681
- 773
Wana Jamii Forums Salaam. Natumai kila mtu ameshakifuta vumbi kichinjio chake tayari kwa ajili ya kesho.
Nimekuwa nikiona matangazo mbalimbali ya watu kuagiza Bidhaa mbalimbali toka nje ya nchi. Kiukweli yale matangazo yamekuwa yakivuta attention ya watu na wengine wamekuwa wakijitosa na kuagiza bidhaa nje ya nchi mimi nikiwa mmoja wapo.
Kuna waagizaji ambao ni maarufu na wengine ambao sio maarufu. Mimi niliwahi kufanya biashara na bwana mmoja maarufu saana humu ndani ambaye anaagiza bidhaa toka nje ya nchi na mara nyingi ukitaka kuagiza bidhaa kutoka Ebay au Amazon huwa ana recommend akuagizie kupitia Ali Express.
Mwaka jana nilikuwa na shida. Kutokana na reputation ya yule bwana nikaamua kufanya nae mawasiliano na kumuomba aniagizie samsung S9+ kwa kuamini kwamba yeye ni mzoefu na hawezi fanya utapeli wa aina yoyote.
Nilimpatia link ya simu niliyokuwa naitaka toka ebay ila akanishauri aniagizie toka Aliexpress. Nilimkubalia kwa sababu nilitokea kumwamin saana kupitia post zake humu ndani. Baada ya kumpa jina la simu na rangi niliyotaka
Sikujihangaisha tena na kila kitu nilimwachia amalize yeye. Gharama ya simu mpaka kunifikia mkononi ilikuwa milioni moja na laki mbili na elfu arobaini. Nililipa pesa zote bila baki kupitia Tigo pesa.
Baada ya miezi miwili ya kusubiri nilipokea mzigo wangu wa simu ukiwa umefungwa vizuri. Ilikuwa ni samsung s9 plus kwa nje. Kwa kuwa ilikuwa ni mpya nilitegemea high performance lakini cha ajabu ile simu ilianza kupata joto kubwa kwa nyuma na ilikuwa inaishiwa chaji baada ya masaa manne au matano regardless matumizi. Nilijaribu kuwasiliana na jamaa yangu mmoja ambae pia alikuwa anatumia simu kama ile kutaka kujua huenda ni tatizo la simu kwa ujumla lakini jamaa aliniambia simu yake ilikuwa haipati joto na akichaji asubuhi inadumu na chaji mpaka jioni.
Nilijaribu kugoogle maneno yaliyoko nyuma ya simu ambayo huwa yanaonyesha model pamoja na manufacturer wa simu. Nilikuja kugundua ile simu ilikuwa ni clone/fake na ilitakiwa kuuzwa angalau laki 4 au 3. Niliumia saana lakini sikuwa na cha kufanya.
Jamaa aliyenifanyia hivi ni maarufu saaaana humu ndani kwenye haya mambo ya uagizaji wa bidhaa toka nje ya nchi ila Kesho tukapige kura tu.