Utapeli nafasi za kazi Game Supermarket Mlimani City

computerkiddy

JF-Expert Member
Oct 1, 2015
479
1,000
Habari wana JF. Kuna mabango yametapakaa yakitangaza nafasi za kazi Game Supermarket Mlimani City wameweka contact zao hizi hapa 071080516 ambaye anajifanya Meneja mwajiri na mwingine huyu hapa ni 0657785895 ambaye ni Supervisor

Ukimpigia Meneja Mwajiri anakwambia nafasi zimeisha ila nitakuombea kwa Supervisor akupe kazi ila form ni elf 15 anakupa namba ya Supervisor. Ukimpigia Supervisor anakwambia fomu ni elfu kumi na tano tuma hela nikuchukulie sasa hivi nipe na majina yako matatu nikuingize kwenye sysytem ya malipo.

Ukimwambia nataka nije mwenyewe nilipe fedha taslimu anasema huwezi wahi nafasi. Kwa waliotuma jina la Tigopesa limesajiliwa kama Judith Jackob, na kwa waliotuma ukishatuma utaambiwa Supervisor amesema hawezi kuingiza majina kwenye system mpaka ujaze fomu ila nimekuombea amesema mpaka utoe elfu ishirini otherwise nkurudishie hela yako.

Ukituma hela anakwambia kesho njoo Mlimani City saa nne. Ikifika saa nne anakwambia nisubir hapo hapo nakuja. Ndo ntolee haji na simu hapokei.

Kuweni makini na utafutaji kazi usikubali kutoa hela kabla ya kupata kazi

Vyombo vya usalama fanyeni kazi yenu
 

loliondokwetu

JF-Expert Member
Feb 21, 2018
581
500
Bora wewe elfu kumi na tano, mimi hyo Meneja wajiri fake aliniambia nitume elfu hamsini hyo eti ni ya uniform za kazi na ya fomu, alafu kesho saa 4 niwahi ili nijiunge na wengine kuanza kazi rasmi, na kwamba nitachagua kati ya shift ya asubui au ya jion. Nusu nitume yaan kwakuwa alikuwa ni mmama na anaongea kistaarabu na kiupole kweli kwel kumbe ni tapeli.
 

computerkiddy

JF-Expert Member
Oct 1, 2015
479
1,000
Bora wewe elfu kumi na tano, mimi hyo Meneja wajiri fake aliniambia nitume elfu hamsini hyo eti ni ya uniform za kazi na ya fomu, alafu kesho saa 4 niwahi ili nijiunge na wengine kuanza kazi rasmi, na kwamba nitachagua kati ya shift ya asubui au ya jion. Nusu nitume yaan kwakuwa alikuwa ni mmama na anaongea kistaarabu na kiupole kweli kwel kumbe ni tapeli.
pole aisee jamaa ni matapali ila sheria ishachukua mkondo wake
ni wale waliokuwa wanatuma meseji za waganga wa kienyeji,na wale wa ile ile hela tuma kwenye namba hii........
 

computerkiddy

JF-Expert Member
Oct 1, 2015
479
1,000
Ngurue alie nona ni kumtafuna tu...
na we ni mmoja wao nini ..... sauti zao zipo kwenye server za tcra
na simu huwa zinarecord geolocation of any activity related to the cellphone
so ni rahisi kuwatrace just ni couple of minutes tu unakuwa ushawatia mbaroni
 

Smart911

JF-Expert Member
Jan 3, 2014
59,773
2,000
Poleni sana...

Ila kwa akili ya kawaida, mtu humjui, ofisi yake hujaiona, unaongea nae tu kwenye simu ati unaamini kabisa ukimtumia pesa atakuingiza kwenye system ya malipo... umeona wapi mambo kama hayo??

Inachekesha sana... anajuaje wewe kama siyo jambazi.. au unajuaje yeye kama siyo jambazi...


Cc: mahondaw
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom