Utapeli na wizi wa 'showroom' za magari DSM | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Utapeli na wizi wa 'showroom' za magari DSM

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Jaramba, Nov 17, 2008.

 1. Jaramba

  Jaramba Member

  #1
  Nov 17, 2008
  Joined: Oct 27, 2008
  Messages: 20
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hivi karibuni nikiwa nipo Tanzania kwa mapumziko mafupi,niliamua kuuza gari langu kuukuu nililoliagiza kutoka Japan miaka kadhaa iliyopita.Kwa kuwa muda wa mapumziko yangu ulikuwa mfupi sana nikaona nitafute gari mbadala kutoka kwenye "showroom" za hapo Dsm. Nikaamua kununua gari kwa "MAZRUI COMISSIONING AGENT" maeneo ya Kijitonyama.Jamaa ni WEZI,MATAPELI na WANAFIKI ingawa wanajidai ni wachamungu sana. Makubaliano yalikuwa wao wangeshughulikia mambo yote ya usajili TRA na ndani ya siku nne kila wangekuwa wameshamaliza kila kitu. Sikuamini imechukua zaidi ya mwezi gari kusajiliwa!! Hakuna sababu ya msingi wanayotoa zaidi ya porojo na uongo,cha kusikitisha ni pale usajili ulipokamilika,wakakabidhi faili lenye nyaraka zote zinazohusiana na hilo gari,kijana wangu alipokuwa anakagua nyaraka akashangaa kukuta tofauti ya mailage (kms),wakati gari inaonyesha imetembea kms.52,000,nyaraka za ukaguzi huko Japan zinaonyesha gari hiyohiyo ilikaguliwa April 2008 likiwa limetembea kms 131,000.Ina maana kuna usanii wa kuchezea mailage ili mteja uamini umenunua gari lililokwenda kms chache kumbe hali halisi ni tofauti!Nikiwa nawasiliana na mwanasheria ili niwafungulie kesi,nimeona si vibaya nikiwatahadharisha wananchi wenzangu na huu utapeli/wizi wa kimachomacho.Naomba tusambaze ujumbe huu kwa watu wengi ili wote tuwe makini.MAZRUI NI WEZI!!!
   
 2. Bowbow

  Bowbow JF-Expert Member

  #2
  Nov 17, 2008
  Joined: Oct 20, 2007
  Messages: 545
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Mkuu Nashukuru kwa huu ujumbe.

  Katika hali ya kawaida usajili wa gari unachukua siku mbili ama tatu kama kila kitu kipo sahihi. Kuchukua mwezi mzima lazima kuna mambo yalikua yanafanywa either hawakulipa kodi kabisa, ama hiyo gari ya wizi so umepewa kanyaboya kwa maana record za gari uliyopewa ni tofauti na gari halisi/???? ama ni wahuni tu.

  Kuna kitengo TRA cha kuomba status ya gari unaenda na copy ya Road license yako( sticker unayopewa kwa ajili ya kubandika kwenye kioo) watakuambia kama imelipiwa ushuru, kama kuna tatizo lolote ambalo wao walishaambiwa watakujulisha na hapo unaweza kuwachukulia hatua zaidi hao wandugu. Ni hayo tu
   
 3. Shadow

  Shadow JF-Expert Member

  #3
  Nov 17, 2008
  Joined: May 19, 2008
  Messages: 2,908
  Likes Received: 71
  Trophy Points: 145
  Duh! Hiyo ndo Bongo Darisalaaam...umecheki na engine yake? Inabidi ukague vizuri ... hayo ndo mamboz ya kina Dudez.

  Kazi kweli kweli next time agiza gari mwenyewe kutoka Japan.
   
 4. MyTanzania

  MyTanzania Senior Member

  #4
  Nov 17, 2008
  Joined: Sep 9, 2008
  Messages: 107
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Ebwana hizi showroom tumezishtukia siku nyingi,wanapata pesa wasiyoitolea jasho ndiyo maana kila siku unawasikia wakidhamini bendi ili japo waimbwe.
  Kwa ushauri,Kuagiza gari japan ni rahisi sana tuache kununua kwa wahuni hawa.Japo inachukua muda kidogo kupata gari lako lakini unapata angalau kitu cha uhakika.
   
 5. Dark City

  Dark City JF-Expert Member

  #5
  Nov 17, 2008
  Joined: Oct 18, 2008
  Messages: 16,277
  Likes Received: 241
  Trophy Points: 160
  Exactly Bongo Darisalama! Kila kitu ni ujanja ujanja na wizi.

  Nadhani usihangaike kuwapeleka mahakamani. Mwone mwanasheria wako muwachimbe mkwara wakupe pesa yako na fidia ya usumbu uagize gari JP. Ukiwapeleka mahakamani watalipa hiyo hela waliyokuibia na issue yako itapata suluhu 2015 wakati tunachacharika na uchaguzi!!!

  Ingawa JP nao wana usanii kidogo ila unapata kitu cha maana! Hizi gari za Bongo na zile zinazotoka Dubai ni kanyaboya (vimeo tupu!!). Jambo la kusikitisha ni kuwa WaTz tunajichimbia kaburi kwa kupoteza imani ya wateja! Watu wataendelea kuabudu na kununua bidhaa za nje (hasa uropa) kuliko za kwetu, hata kwa vitu vidogo kama nyembe na pini!!
   
 6. zomba

  zomba JF-Expert Member

  #6
  Nov 19, 2008
  Joined: Nov 27, 2007
  Messages: 17,081
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 0
  Nakupa pole kwa hilo, na mara nyingine uwe makini sana na hawa jamaa wa ma-showroom, binafsi nam-recommend jamaa mmoja wa Kariakoo anaitwa Abdul, mara nyingi hujitangaza katika Advertising Dar. Huyu anakuagizia gari kutoka Japan na anakupa data zote kabla hajaileta na gharama zake ni nafuu kweli. Utampata katika 0754-484384. Mwambie Dar. ndie aliempigia debe.
   
 7. Masanilo

  Masanilo JF-Expert Member

  #7
  Nov 19, 2008
  Joined: Oct 2, 2007
  Messages: 22,303
  Likes Received: 168
  Trophy Points: 160
  JF Tangazo la biashara, if the worse get into worst wafanyabiashara wengi wa Dar ni matapeli, kuna jamaa yangu alimlalamika pia kuhusu huyu Abdul.
   
 8. Yona F. Maro

  Yona F. Maro R I P

  #8
  Nov 19, 2008
  Joined: Nov 2, 2006
  Messages: 4,237
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 0
  Utakuwa mwana si wako
   
 9. Yona F. Maro

  Yona F. Maro R I P

  #9
  Nov 19, 2008
  Joined: Nov 2, 2006
  Messages: 4,237
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 0
  can u imagine ni watu wangapi wameshapiga hiyo namba ? mpaka sasa hivi na pengine kuingia mkataba kabisa na amemhusisha na advertising dar - pale advertising dar wameshaandika kabisa sheria zao kuhusu biashara hizi
   
 10. Kibunango

  Kibunango JF-Expert Member

  #10
  Nov 20, 2008
  Joined: Aug 29, 2006
  Messages: 7,635
  Likes Received: 180
  Trophy Points: 160
  Kwa maneno mengine unataka kutoa ujumbe gani?
   
 11. Fidel80

  Fidel80 JF-Expert Member

  #11
  Nov 20, 2008
  Joined: May 3, 2008
  Messages: 21,976
  Likes Received: 104
  Trophy Points: 145
  duh si mchezo naye ni dudez balaa juu ya balaa.
  Bora uwaone AUTOREC nao vp?wanaofisi zao samora pale.
   
 12. Mtaalam

  Mtaalam JF-Expert Member

  #12
  Nov 20, 2008
  Joined: Oct 1, 2007
  Messages: 1,277
  Likes Received: 40
  Trophy Points: 145
  hiyo ndo bongo darisalaaaam.....akili kumkichwa ukilemaaa umeachwa feri
  aliyeuziwa cheni katoa hela bandia,na aliyetoa hela kapewa cheni bandia!!
  hapo sasa
   
 13. Masanilo

  Masanilo JF-Expert Member

  #13
  Nov 20, 2008
  Joined: Oct 2, 2007
  Messages: 22,303
  Likes Received: 168
  Trophy Points: 160
  Fidel80

  Dudez Mstaraabu, unajua sisi wa bongo wakati mwingine tunapenda slope sana ( Y increase over X increase) Abdul anachokifanya nikuagiza kupitia website, kitu ambacho mtu yeyote anaweza kukifanya. Anaweka faida yake anakukabidhi goma lako, Abdul Aliisha mdhulumu mdada mmoja Kastarlet kake hadi leo wansumbuana, bora uagize kwenye kampuni kubwa kama Autorec ama V.WEST co. Kuweni makini na kampuni za kwenye mifuko ya Rambo.
   
 14. Njowepo

  Njowepo JF-Expert Member

  #14
  Nov 20, 2008
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 9,297
  Likes Received: 381
  Trophy Points: 180
  Booooongo Eeeeeh Bongo Darisalaaaama utalialial ndani ya Darisalama x3 nakumbuka wimbo wa Lady Jay D
   
 15. Kaa la Moto

  Kaa la Moto JF-Expert Member

  #15
  Nov 20, 2008
  Joined: Apr 24, 2008
  Messages: 7,666
  Likes Received: 164
  Trophy Points: 160
  Kama unataka kununua gari Usipate shida ya kwenda kote huko. Nchini Uganda kuna Yard nyingi sana zinazouza magari yaliyotumika kama Dubai tena kwa gharama kama ya Dubai au tofauti kidogo tu.
  Kwa wajanja waliokwisha jua huwa hawaendi tena mbali huko bali wanakwenda Uganda na unachagua gari yako na kuja kuilipia tax na duty kisha unakuja unaendesha nyumbani.
  Epukana na matapeli wa Dar hao.
   
 16. Mwiba

  Mwiba JF-Expert Member

  #16
  Nov 20, 2008
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 7,606
  Likes Received: 215
  Trophy Points: 160
  Gharama zote za kununua gari hapa Dar zinaweza zikakupeleka Japani na kurudi na karandinga.Na wako jamaa wa Kipemba kule wanazungumza hata kijapani wa takupeleka kwenye minada na vichochoro vinavyouza magari utajichagulia kwa nafasi yako.
   
 17. bokassa

  bokassa JF-Expert Member

  #17
  Nov 20, 2008
  Joined: May 19, 2007
  Messages: 403
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Au agizieni kupitia

  Bokassacomissioningagent

  Hawa jamaa wazuri sana, Ofisi zao ziko mtaa wa luthuli pale daresalama!!!!!!
   
 18. M

  Mama JF-Expert Member

  #18
  Nov 20, 2008
  Joined: Mar 24, 2008
  Messages: 2,858
  Likes Received: 20
  Trophy Points: 0
  Mzee mwenzangu hapa sikubaliani na wewe.

  Kwako pakiharibika ni wajibu wako kupatengeneza na sio kuhamia kwa jirani.
   
 19. H

  Hofstede JF-Expert Member

  #19
  Nov 20, 2008
  Joined: Jul 15, 2007
  Messages: 3,584
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 0  Hakuna haja ya kumtumia mtu kuagiza gari Japan, kuna makampuni yayoeleweka Dar ambayo unayapa katika mtandao na kumalizana nayo. Kampuni nyingi za kijapan zina wawakilishi Dar, we waone hao hao unaagiza mwenyewe kwenye mtandao bila commission wala mission town. Usimuamini mbongo yoyote kukuagizia gari, Utamaduni wetu umebadilika sana kila kitu mtu anaona deal.

  Mimi niliagiza gari Japan mwenyewe kupitia kwenye mtandao wa AUTOREC tena nikiwa nje ya Tanzania na gari lilifika likiwa salama na nililipeleka jamaa wakalicheki lipo safi na mpaka leo lipo quality.

  Nilitumia wiki kulitoa bandarini na siku tatu registration. Tusipende mkato ndugu zangu. Show room nyingi Bongo ni kanyaboya, watu wanaendesha magari yao bongo yakipata mzinga wanayatengeza na kurudisha showroom.

  Yaani mimi mentali yangu ni kwamba mbongo don't trust hata kidogo tumekuwa kunguru kinoma kila mtu anataka kuwa tajiri kwa shortcut. Mpaka tutakapokuja kujua kuwa Biashara ni uhusiano, kwamba ukiniuzia kizuri leo na kesho nitakuja tena au kumleta mtu ndiyo tutakapokuwa na sustainable businesses.

  Vinginevyo hizi showroom zote zitakufa kifo cha kawaida kwa kuji-demarket na ujanja wao wa kupata leo hawaangalii future.
   
 20. mhalisi

  mhalisi JF-Expert Member

  #20
  Mar 30, 2014
  Joined: Sep 9, 2011
  Messages: 1,181
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 0
  mimi huwa sina imani kubwa na show room za magari hapa nchini.
   
Loading...