Tomaa Mireni
JF-Expert Member
- Sep 8, 2015
- 2,328
- 2,283
Ukiwa wakala wa huduma za kipesa unakua unafanya miamala mingi sana kwa siku kiasi kwamba huenda mingine usiikumbuke kama hukuandika kwenye daftari.
Airtel Money wao hawana log book kwa kumbukumbu za mteja. Matapeli wanapitia humu humu sababu wanajua hukuandika.
Alikuja mteja kama siku ya jana akaomba kuwekewa mfano 5000 ukamwekea vizuri na kuondoka zake sababu ya shughuli nyingi huwezi kufika kesho ukakumbuka wateja wote na kiasi ambacho uliwawekea.
Kesho anarudi mida ya mchana anadai alikupa 50,000 hesabu ya bosi wake kwenye boda boda ukamwekea 5,000 tu. Hapo hakuna mwenye uhakika na madai ya mwengine wewe unaweza kusema niliweka yote. Anadai bosi wake anamsumbua anataka hesabu yake kamili ambayo alileta jana.
Haraka haraka utapiga simu Airtel ili kuthibitisha madai ya mteja huyo. Utajibiwa kuwa ni kweli jana muda fulani ulimuwekea kiasi cha 5,000 tu huyo mteja. Mpaka hapo kama kichwa kibovu unapigwa sababu utalazimika kummaliza 45,000 yake iliyobaki.
Jambo muhimu la kuzingatia na kufanya:
WAKALA HAKIKISHA HESABU YAKO YA MZUNGUKO UNAIJUA KIKAMILIFU NA IKIWEZEKANA UMEIANDIKA SEHEMU
1. Mwambie huyo mteja kuwa kwa sababu unajua jumla ya kiasi chako cha pesa kinachozunguka ngoja upige hesabu.
2. Piga hesabu zako uone kama kuna kiasi halisi kwenye mzunguko wako.
3. Mwambie kiasi kilichopo kwenye mzunguko wangu hakijaongezeka kwahiyo jana alitoa kiasi hicho hicho alichowekewa. Yeye mwenyewe ataondoka kwa kisingizio cha kwenda kumuita boss wake ili aje na simu na ujumbe wa muamala.
Kama hakubaliani na unachomwambia achukue hatua zaidi kwa sababu biashara ni siri huwezi kumwambia una jumla ya shilingi ngapi kwenye mzunguko wako. Labda kwa usaidizi wa polisi kama itahitajika.
Kama una tabia ya kuchanganya pesa za miamala na pesa za biashara nyingine huenda ukashindwa kwenye utapeli huo kama mtu atakomaa.
Sent using Jamii Forums mobile app