Utapeli mpya mjini | Mawakala wa huduma za kifedha kuweni makini sana

Tomaa Mireni

JF-Expert Member
Sep 8, 2015
2,328
2,283
Ukiwa wakala wa huduma za kipesa unakua unafanya miamala mingi sana kwa siku kiasi kwamba huenda mingine usiikumbuke kama hukuandika kwenye daftari.

Airtel Money wao hawana log book kwa kumbukumbu za mteja. Matapeli wanapitia humu humu sababu wanajua hukuandika.

Alikuja mteja kama siku ya jana akaomba kuwekewa mfano 5000 ukamwekea vizuri na kuondoka zake sababu ya shughuli nyingi huwezi kufika kesho ukakumbuka wateja wote na kiasi ambacho uliwawekea.

Kesho anarudi mida ya mchana anadai alikupa 50,000 hesabu ya bosi wake kwenye boda boda ukamwekea 5,000 tu. Hapo hakuna mwenye uhakika na madai ya mwengine wewe unaweza kusema niliweka yote. Anadai bosi wake anamsumbua anataka hesabu yake kamili ambayo alileta jana.

Haraka haraka utapiga simu Airtel ili kuthibitisha madai ya mteja huyo. Utajibiwa kuwa ni kweli jana muda fulani ulimuwekea kiasi cha 5,000 tu huyo mteja. Mpaka hapo kama kichwa kibovu unapigwa sababu utalazimika kummaliza 45,000 yake iliyobaki.

Jambo muhimu la kuzingatia na kufanya:

WAKALA HAKIKISHA HESABU YAKO YA MZUNGUKO UNAIJUA KIKAMILIFU NA IKIWEZEKANA UMEIANDIKA SEHEMU

1. Mwambie huyo mteja kuwa kwa sababu unajua jumla ya kiasi chako cha pesa kinachozunguka ngoja upige hesabu.

2. Piga hesabu zako uone kama kuna kiasi halisi kwenye mzunguko wako.

3. Mwambie kiasi kilichopo kwenye mzunguko wangu hakijaongezeka kwahiyo jana alitoa kiasi hicho hicho alichowekewa. Yeye mwenyewe ataondoka kwa kisingizio cha kwenda kumuita boss wake ili aje na simu na ujumbe wa muamala.

Kama hakubaliani na unachomwambia achukue hatua zaidi kwa sababu biashara ni siri huwezi kumwambia una jumla ya shilingi ngapi kwenye mzunguko wako. Labda kwa usaidizi wa polisi kama itahitajika.

Kama una tabia ya kuchanganya pesa za miamala na pesa za biashara nyingine huenda ukashindwa kwenye utapeli huo kama mtu atakomaa.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ngoja nirudi kwa yule jamaa jana niliweka elfu hamsini nikamwambie mbona katuma elfu hamsini baada ya laki tano tena naenda na polisi ili kuhalalisha zaidi.
 
Huna hata haja ya kupiga hesabu hapo, kwa kawaida mteja anatakiwa apate confirmation sms kabla hajamalizana na wakala. Kama ulimwekea nae akathibitisha kuwa tayari imeingia ndio imeisha hivyo.
 
Swali nje ya mada:-

Nikiwa na 1,000,000 kwenye line ya M-Pesa nikaihudumu kwa wateja (kuweka) nitapata gawio la sh. ngapi toka kwa service provider?
 
kuna ile unakuta unampa mteja simu aandike namba, yeya anaingia kwenye sms anaangalia sms ya mwisho ya muamala anaituma kwenye no yake then anaisave no yake kwnye cm ya wakala M-PESA akimaliza anakurudushia cm anajifanya ameahurisha kuweka ela,

mfano kulikwa na balance ya sh 50000 anaedit ile sms kuwa ametia sh 40000 salio lako jipya ni sh 10000, alafu anaituma hiyo sms kwenye ile cm ya wakala ambayo alisave no yake jina ni M-PESA
 
kuna ile unakuta unampa mteja simu aandike namba, yeya anaingia kwenye sms anaangalia sms ya mwisho ya muamala anaituma kwenye no yake then anaisave no yake kwnye cm ya wakala M-PESA akimaliza anakurudushia cm anajifanya ameahurisha kuweka ela, mfano kulikwa na balance ya sh 50000 anaedit ile sms kuwa ametia sh 40000 salio lako jipya ni sh 10000, alafu anaituma hiyo sms kwenye ile cm ya wakala ambayo alisave no yake jina ni M-PESA
Hii kuna jamaa angu amepigwa laki 6 wiki iliyopita.

Kuna jamaa alikuja akaomba awekewe elfu 5, akaweka ila kabla hajaondoka akaja mtu mwingine akaomba atume/kuweka elfu 50, sasa huyu wa kwanza akawa anampigisha story yule mtoa huduma tena kuhusu mambo ya Corona na story zilikuwa tamu sana, basi mtoa huduma akampa simu yule mteja wa pili ili aweke namba za simu. Alichokifanya jamaa ni kwenda 'inbox' akajitumia sms na kisha akasave namba yake kama TIGOPESA kwenye simu ya mtoa huduma. Jamaa akarudisha simu na kumuambia muamala umekatika.

Mtoa huduma akafanya tena muamala na kufanikisha kutuma hela kwa mteja. Yule jamaa wa kwanza akachukua simu kwa jamaa wa pili na kumuambia mtoa huduma anatoa laki 6, kumbe aliedit ile sms ya salio la mwisho akaongeza laki 6 na kwa kuwa kule hii namba ikiseviwa kwa jina la TIGOPESA basi jamaa akatuma sms ya kawaida lakini kule kwa mtoa huduma likatokea jina la TIGOPESA kuwa amepokea laki 6 na salio jipya ni kadhaa, mtoa huduma si akaingia king akampa laki 6.

Nimekuwa nasoma visa vya kuibiwa kwenye hizo mobile money transactions na nimegundua wizi mwingi hutokea kwa sababu biashara hizi huendeshwa ki-local, kimazoea na kizembe sana. Kwa nini watu wasiwe organized jamani watanzania tuna laana gani? Kwa nini mtu asiwe na counter book ambayo mteja atarekodi details zake kabla ya kuhudumiwa? Vitu kama namba anayotuma fedha kweli unampa aandike mwenyewe? Kwa nini kusiwe na karatasi akaandika namba halafu mhudumu akaingiza mwenyewe kwenye simu?
 
Huna hata haja ya kupiga hesabu hapo, kwa kawaida mteja anatakiwa apate confirmation sms kabla hajamalizana na wakala. Kama ulimwekea nae akathibitisha kuwa tayari imeingia ndio imeisha hivyo.
Alidai anamwekea bos wake yupo nyumbani na simu ya mletaji ilikua haina chaji,alifanya kuuliza "tayari imeenda"? Akipata jibu tayari anaondoka

Sent using Jamii Forums mobile app
 
kuna ile unakuta unampa mteja simu aandike namba, yeya anaingia kwenye sms anaangalia sms ya mwisho ya muamala anaituma kwenye no yake then anaisave no yake kwnye cm ya wakala M-PESA akimaliza anakurudushia cm anajifanya ameahurisha kuweka ela,

mfano kulikwa na balance ya sh 50000 anaedit ile sms kuwa ametia sh 40000 salio lako jipya ni sh 10000, alafu anaituma hiyo sms kwenye ile cm ya wakala ambayo alisave no yake jina ni M-PESA
Iyo wengi wanaijua na kwa sasa wakala hakuna kumpa mteja simu aweke no yake

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hii kuna jamaa angu amepigwa laki 6 wiki iliyopita.

Kuna jamaa alikuja akaomba awekewe elfu 5, akaweka ila kabla hajaondoka akaja mtu mwingine akaomba atume/kuweka elfu 50, sasa huyu wa kwanza akawa anampigisha story yule mtoa huduma tena kuhusu mambo ya Corona na story zilikuwa tamu sana, basi mtoa huduma akampa simu yule mteja wa pili ili aweke namba za simu. Alichokifanya jamaa ni kwenda 'inbox' akajitumia sms na kisha akasave namba yake kama TIGOPESA kwenye simu ya mtoa huduma. Jamaa akarudisha simu na kumuambia muamala umekatika.

Mtoa huduma akafanya tena muamala na kufanikisha kutuma hela kwa mteja. Yule jamaa wa kwanza akachukua simu kwa jamaa wa pili na kumuambia mtoa huduma anatoa laki 6, kumbe aliedit ile sms ya salio la mwisho akaongeza laki 6 na kwa kuwa kule hii namba ikiseviwa kwa jina la TIGOPESA basi jamaa akatuma sms ya kawaida lakini kule kwa mtoa huduma likatokea jina la TIGOPESA kuwa amepokea laki 6 na salio jipya ni kadhaa, mtoa huduma si akaingia king akampa laki 6.

Sent using Jamii Forums mobile app
Kuna tapel kanipigia simu juz anadai ni mtoa huduma wa tigo na anaskiliza changamoto za mawakala kumbe tapeli

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Watu wa mitandao wanapoweka sheria ni za kukulinda wewe pia, ungefuata utaratibu wala usingepata hasara
Binafsi sijapata hasara na hata kama nisingepiga hesabu nisingempa kwa sababu alitakiwa kuja na simu au kurud jana ile ile.

Kwa kawaida hata bank ukishaondoka counter basi kila kitu chako kiko poa ukirudi baadae unataka mwengine

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom