Wana JF,
Ninapenda kuchukua fursa hii nilete uzi huu kuhusu utapeli mpya ulioibuka hasa katika minada ya simu inayofanywa maeneo ya wazi kama stendi ya basi.Nimeshuhudia hili nilipokuwa Morogoro.Hawa jamaa wajanja sana.Wanachofanya ni kwamba wanapita mitaani na gari wakiwatangazia wananchi na kipaza sauti kwamba kutakuwa na mnada wa hadhara baada ya kukamata mali ya mdaiwa.Matapeli hawa mara nyingi hujifanya kampuni ya udalali iliyopewa dhamana ya kuuza mali za mdaiwa.
Matapeli hawa hushirikiana na mwenye duka.Huvamia duka la huyo mfanyabiashara wanaojifanya ameshindwa kulipa deni na kuchukua simu zote.Kabla hawajavamia huchukua simu mbovu zilizovyalishwa hauzing mpya na kuziweka dukani.Kisha huvamia duka na kuzipiga mnada wa hadhara simu mbovu hizo tena kwa bei kubwa.Mara nyingi simu hizi copy ya simu maarufu za smart phone kama Samsung,Nokia,Techno na nyingine.
Wengi walionunua simu hizi mnadani wamelia baada ya kugundua ni vimeo.Kwa hiyo tusiamini minada hii ya stendi za mabasi kwani ni magumashi tupu.