Utapeli mpya katika minada ya simu

mbeyaman

Member
Sep 28, 2013
97
0
Wana JF,
Ninapenda kuchukua fursa hii nilete uzi huu kuhusu utapeli mpya ulioibuka hasa katika minada ya simu inayofanywa maeneo ya wazi kama stendi ya basi.Nimeshuhudia hili nilipokuwa Morogoro.Hawa jamaa wajanja sana.Wanachofanya ni kwamba wanapita mitaani na gari wakiwatangazia wananchi na kipaza sauti kwamba kutakuwa na mnada wa hadhara baada ya kukamata mali ya mdaiwa.Matapeli hawa mara nyingi hujifanya kampuni ya udalali iliyopewa dhamana ya kuuza mali za mdaiwa.

Matapeli hawa hushirikiana na mwenye duka.Huvamia duka la huyo mfanyabiashara wanaojifanya ameshindwa kulipa deni na kuchukua simu zote.Kabla hawajavamia huchukua simu mbovu zilizovyalishwa hauzing mpya na kuziweka dukani.Kisha huvamia duka na kuzipiga mnada wa hadhara simu mbovu hizo tena kwa bei kubwa.Mara nyingi simu hizi copy ya simu maarufu za smart phone kama Samsung,Nokia,Techno na nyingine.

Wengi walionunua simu hizi mnadani wamelia baada ya kugundua ni vimeo.Kwa hiyo tusiamini minada hii ya stendi za mabasi kwani ni magumashi tupu.
 
Tiger One

JF-Expert Member
Apr 11, 2012
568
500
Huo ni wizi Wa vijijini kwani mjini utamuuzia nani cm za minadani? Ahsante kwa kuwasaidia wagalatia vijinini.
 
Kurunzi

JF-Expert Member
Jul 31, 2009
5,984
2,000
Pale mwenge kuna jamaa wanalizwa kila siku kwa kuuziwa simu mbovu
 
KRISTIAN P

JF-Expert Member
Feb 16, 2013
352
225
Pale mwenge kuna jamaa wanalizwa kila siku kwa kuuziwa simu mbovu

Ni kweli mkuu ata mm nimeshawaona Mwenge Stand.. Matapeli wanauza simu bila battery,kwa iyo km ukinunua simu badae wanakuzia simu. Ukingundua simu mbovu imekula kwako..
 
Mwanamageuko

JF-Expert Member
Oct 31, 2010
7,633
2,000
na minada hiyo inawezekana si rasmi ama si kampuni za minada lakini ndio hivyo watawala na sekta zao husika wangali usingizini na hawamjali mtanzania...

Maswali:
Hao wafanya minada wako maeneo rasmi au ni kama wamachinga?
Kama hawako maeneo rasmi je kwanini hawaondolewi maeneo hayo?

Naomba msaada wa majawabu hapo.
 
mathabane

JF-Expert Member
Jan 27, 2013
2,244
2,000
Acheni ushamba nyie, tangu lini mnadani zikauzwa electronic devices badala ya dukani? Mnadani wanauzwa ng'ombe na mbuzi zaidi ya hapo wizi mtupu.
 
sajumo

JF-Expert Member
Nov 20, 2013
1,793
2,000
huu wiz usha ekspaya kama karata tatu ila ni kwa sisi watu wa uswahili ambao tuna masters na phd za kitaologia d knob anita ya mtaa poleni kwenu maisha laini
 
mbabimbabi

Member
Jun 21, 2014
38
0
Wana JF,
Ninapenda kuchukua fursa hii nilete uzi huu kuhusu utapeli mpya ulioibuka hasa katika minada ya simu inayofanywa maeneo ya wazi kama stendi ya basi.Nimeshuhudia hili nilipokuwa Morogoro.Hawa jamaa wajanja sana.Wanachofanya ni kwamba wanapita mitaani na gari wakiwatangazia wananchi na kipaza sauti kwamba kutakuwa na mnada wa hadhara baada ya kukamata mali ya mdaiwa.Matapeli hawa mara nyingi hujifanya kampuni ya udalali iliyopewa dhamana ya kuuza mali za mdaiwa.

Matapeli hawa hushirikiana na mwenye duka.Huvamia duka la huyo mfanyabiashara wanaojifanya ameshindwa kulipa deni na kuchukua simu zote.Kabla hawajavamia huchukua simu mbovu zilizovyalishwa hauzing mpya na kuziweka dukani.Kisha huvamia duka na kuzipiga mnada wa hadhara simu mbovu hizo tena kwa bei kubwa.Mara nyingi simu hizi copy ya simu maarufu za smart phone kama Samsung,Nokia,Techno na nyingine.

Wengi walionunua simu hizi mnadani wamelia baada ya kugundua ni vimeo.Kwa hiyo tusiamini minada hii ya stendi za mabasi kwani ni magumashi tupu.

Mnarudisha nyuma maendeleo ya nchi bhana, simu haina stakabadhi wala guarantee bado upo tu ili upate cheap, haaya nunueni!!?? .
 
1gb

JF-Expert Member
Jun 30, 2013
1,840
2,000
Mkuu wala sio Utapeli Mpya,mbona upo tangu kitambo.
Au ww ndo kwanza umeuona?
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Similar Discussions

Top Bottom