Utapeli Mpaya: Jinsi wadada wa mjini wanavyotapeliwa na mabloo wa Ulaya

Jaalut

Member
Jan 18, 2020
72
244
Picha linaanza pale mitaa ya instagram, mdada anakutana na bloo ana picha kali kichizi kwenye insta yake, picha zinaonesha kwamba jamaa yuko ulaya alafu anakula bata kichizi yani kwa kutazama picha jamaa sio mtu wa njaa kabisa.

Bloo anazama DM kwa mdada na baadae wanaanzisha urafiki, bloo anakuwa anampigia simu uyo demu na namba inaonesha ni ya nje ya nchi wakat uyo bloo yuko bongo

Bloo atamwambia mdada kwamba anataka kumtumia zawadi, mara nyingi inakuwa simu kali tena mpya kabisa simu yenyewe ni iphone tena ile ya bei juu yani kitu orijino

Ilikusibitisha kwamba hatanii basi bloo atamtumia picha Yule demu , picha za mazawadi anayotaka kumtumia.

Kesho yake bloo atamtumia tena picha Yule mdada kwamba yuko DHL anamtumia simu yake na mazawadi mengine
Basi mzee baba baada ya hapo atamcheki tena Yule dada na kumwambia tayali keshamtumia zawadi zake na asubili simu toka watu wa DHL watampa maelekezo ya kufanya

Kesho yake mida ya asubuhi mdada atapigiwa simu na mtu atakaye jitambulisha kama mfanyakazi wa DHL
Atamwambia kwamba mzigo wake umefika lakini haujalipiwa ushuru, watamtajia kiasi cha pesa ambacho inabidi alipe ili kesho akachukue mzigo wake

Bloo akija kuumbiwa kwamba mzigo wanasema haujalipiwa ushuru atamwambia kwamba yeye alishindwa kulipia sababu kadi yake ya benki inazingua , si unajua tena ulaya sistimu zake ni malipo kwa kadi au atampa sababu yoyote tu ilimladi aingie king

Mara nying demu atakuwa anajistukia kumwambia jamaa kama mzigo haujalipiwa kodi sababu jamaa katoa pesa kibao ili amtumie yeye zawad kwaiyo inabidi tu nay eye ajiongeze ili apate zawadi zake

Wale jamaa wa DHL feki watamwambia inabidi alipie ule mzigo kupitia namba ya simu, watampa namba ya simu na akishalipia tu basi apo ndo imekula kwake, yani anakuwa kapigwa changA kwa tamaA zake

inakuwa ngumu kustuka kwa sababu zifuatazo

- bloo anakuwa anatumia namba ya nje ya nchi, yani apa anakuwa amenunua namba ya nchi ya ulaya kwenye mtandao na anaitumia kutapeli
- wabongo wengi hatujawai tumia DHL kwaiyo inakuwa rahisi kupigwa changa

kama mdada anakuwa mtu wa tamaa na kupenda vitu vya bure basi lazima anase katika mtego huu

-wabongo bado tunazile fikra kwamba mtu akiishi ulaya basi anakuwa na pesa ndefu

kuweni makini wapwa...mjini shule

By profesa from twitter...

IMG_20200628_094622.jpg
 
kuna wakati mwingine mtu unajiweka mwenyewe kwenye mazingira ya kutapeliwa.maswali ni mengi ila kitu kikubwa cha kujiuliza unawezaje kumtumia pesa mtu usiemjua,kisa tu kakupigia simu kuwa yeye ni afsa wa DHL?
 
Hizo fedha wanazopigwa wanakuwa wamezipiga mahali.
kuuziana dhahabu fake kwa Dollar fake.
 
Ni "bloo" kama mleta mada alivosema labda wewe umeshindwa kuelewa hii trend ya Mabloo siku hizi.
Bro= brother = kaka.
Bloo = ni kijana wa makamo(wakiume) ambae yuko na connection mjini na pia anandinga yake na anaishi kwenye apartment Kali.
Mpwa = ndo kama Mimi jobless ambae napambana niwe bloo
Na Blazaaaa??
 
Mality yala from dark Senegal alinijaribu na hakika nilinuka kisawasawa.

Hapo nilikuwa chuo zamani hizo nikapokea Email ya huy bidada akihitaji msaada wa kumuhifadhi aje tz kula maisha na pesa alizoachiwa na dingi yake .

Aisee

Na kuniahidi kunitumia vizawadi kadhaa na kweli niliwaza sana lakini nilipata wazo na nikaingia google kuangalia jina la mality yala .

Kumbe ni mtu alikuwa na fedha sana na alishafariki na aliacha fedha kama ulithi kwa binti yake .

Aisee usipokuwa makini wanakuingiza mjini chapu mno
 
Wapumbavu wachache sana wanaweza kukaa kwenye kimtego hicho

Ushuru unalipa TRA, sasa hata kama TRA wanalipwa kupitia mitandao ya simu lakini hakuna malipo ya kulipa bila control number tena kwenda kwenye namba binfsi
 
Back
Top Bottom