Utapeli katika ununuzi wa mashine za kutoa risiti maarufu kama EFD

Crucifix

JF-Expert Member
Feb 20, 2011
1,640
2,000
UTAPELI KATIKA UNUNUZI WA MASHINE ZA KUTOA RISITI MAARUFU KAMA EFD

TRA Tanzania Revenue Authority - TRA wameteua mawakala 10 (walau ndiyo orodha niliyopewa) na mimi nimetembelea mawakala watatu na wote hawana mashine mkononi.

Kinachofanyika; wateja wanalipa 590,000/= kisha mnasubirishwa kwa majuma mawili au matatu. Kwa maneno mengine, tunanunulishwa mashine kwa mtaji wetu wenyewe!
 
Koryo2

JF-Expert Member
Nov 28, 2016
1,648
2,000
Ni vema Serikali ikawa na Kampuni ya kizalendo itakayosimamia EFD machines. Kuna tatizo kubwa na mawakala. Kila ukipeleka tatizo dogo tu lazima utoe hela. Juzi juzi mashine yangu ilikuwa haitoi herufi inayosomeka wakaniomba 150,000 ili kurekebisha tatizo hilo.

Hili ni tatizo dogo lakini waliniomba hela ndefu. Hawa hawapo kusaidia wafanyabiashara ila kupiga tu hela. TRA wafuatilieni hawa wakala na mhakikishe tunakuwa na Kampuni ya Kitanzania itakayosimamia majukumu ya mashine hizi.
 
Erythrocyte

JF-Expert Member
Nov 6, 2012
81,858
2,000
UTAPELI KATIKA UNUNUZI WA MASHINE ZA KUTOA RISITI MAARUFU KAMA EFD

TRA Tanzania Revenue Authority - TRA wameteua mawakala 10 (walau ndiyo orodha niliyopewa) na mimi nimetembelea mawakala watatu na wote hawana mashine mkononi.

Kinachofanyika; wateja wanalipa 590,000/= kisha mnasubirishwa kwa majuma mawili au matatu. Kwa maneno mengine, tunanunulishwa mashine kwa mtaji wetu wenyewe!
Bora wewe umelipa hiyo hela ndogo , mimi nilinunua mashine 5 kila moja 850000
 
kidadari

JF-Expert Member
Jul 26, 2012
7,810
2,000
Ni vema Serikali ikawa na Kampuni ya kizalendo itakayosimamia EFD machines. Kuna tatizo kubwa na mawakala. Kila ukipeleka tatizo dogo tu lazima utoe hela. Juzi juzi mashine yangu ilikuwa haitoi herufi inayosomeka wakaniomba 150,000 ili kurekebisha tatizo hilo.

Hili ni tatizo dogo lakini waliniomba hela ndefu. Hawa hawapo kusaidia wafanyabiashara ila kupiga tu hela. TRA wafuatilieni hawa wakala na mhakikishe tunakuwa na Kampuni ya Kitanzania itakayosimamia majukumu ya mashine hizi.
Hawa jamaa.walichofanya wanakupa garantee ya mwaka na wanakutengenezea bure ikiharibika.....ngoja mwaka uishe uone wanavuna kwa kwenda mbele maana hakuna wafundi zaidi ya wao
 
Lagrange

JF-Expert Member
Mar 7, 2017
2,088
2,000
Hawa ni wez tu ,hizi kampuni zipo kwa ajili ya kupiga hela ,na huenda ni za hawa hawa vigogo wa serekalini tu,, kama hii 80,000 inayolipwa kwa ajili ya upgrading ni wizi mtupu , kwanini wasi upgrade wenyewe.?
 
Bambushka

JF-Expert Member
Jan 9, 2020
2,037
2,000
Hawa ni wez tu ,hizi kampuni zipo kwa ajili ya kupiga hela ,na huenda ni za hawa hawa vigogo wa serekalini tu,, kama hii 80,000 inayolipwa kwa ajili ya upgrading ni wizi mtupu , kwanini wasi upgrade wenyewe.?
Usisahau wao kazi yao inabakia ya kupiga faini ya kutokutoa risiti wakati wanajua wenzao wamechukua machine ku upgrade!

Everyday is Saturday............................... :cool:
 
Lagrange

JF-Expert Member
Mar 7, 2017
2,088
2,000
Usisahau wao kazi yao inabakia ya kupiga faini ya kutokutoa risiti wakati wanajua wenzao wamechukua machine ku upgrade!

Everyday is Saturday............................... :cool:

Ndio washine ziko kwa wenzao wanapiga hela na wao wako mtaani wanakagua risiti ,wanapiga hela Mara mbili yaan.
 
Champagnee

JF-Expert Member
Jan 12, 2019
5,374
2,000
Hawa ni wez tu ,hizi kampuni zipo kwa ajili ya kupiga hela ,na huenda ni za hawa hawa vigogo wa serekalini tu,, kama hii 80,000 inayolipwa kwa ajili ya upgrading ni wizi mtupu , kwanini wasi upgrade wenyewe.?

Taarifa nayojua kwamba hio 80k itapunguzwa kwenye kodi yako utakayokadiliwa
 
Mnyatiaji

JF-Expert Member
Dec 13, 2018
1,889
2,000
UTAPELI KATIKA UNUNUZI WA MASHINE ZA KUTOA RISITI MAARUFU KAMA EFD

TRA Tanzania Revenue Authority - TRA wameteua mawakala 10 (walau ndiyo orodha niliyopewa) na mimi nimetembelea mawakala watatu na wote hawana mashine mkononi.

Kinachofanyika; wateja wanalipa 590,000/= kisha mnasubirishwa kwa majuma mawili au matatu. Kwa maneno mengine, tunanunulishwa mashine kwa mtaji wetu wenyewe!
Mitaji yetu ndiyo mtaji wao
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom