Utapeli kama huu ukitapeliwa, utapata msaada wapi au ndio utalala nacho?

Mkogoti

TAPELI Mkubwa
May 3, 2020
2,416
3,908
Habari wakuu Mimi mzima kabisa wa afya Natumaini nawe pia huko mzima kabisa, bado Tunaendelea na maombelezo ya Rais wetu Mpendwa Mh. William B. Mkapa R.I.P 😞🙏

Ipo hivi wakuu, nipo nawaza kitu ambacho kipo ubongoni mwangu nimekifikiria tu ghafla.

Ipo hivi Huku Maeneo ninapoishi jina (kapuni) kuna Uwanja wa ndege ulikuwa wa kitambo na ulikuwa unatumika ila sijui nini kilitokea ndege kubwa hazitui tena zinaishia mkoa jirani, bali ni ndege binafsi ndio zinaruhusiwa kutua sikujua ni kwanini.

Basi serikali imeamua tena kuutengeneza uwe mkubwa sasa kuna nyumba zipo baadhi na kiwanja na kuna mashamba pembeni watu walikuwa wanalima mpunga, viazi, na mboga mboga kwa maana hiyo wanatakiwa watoke.

Basi nikawaza hivi mtu ana nyumba yake imepigwa alama ya X yani inatolewa hiyo nyumba na serikali imeshatoa malipo kwa hao wenye nyumba! Halafu sasa huyo mwenye nyumba akafanya ujanja akatafuta mtu wa mbali sana kutoka mkoani akasema anaiuza na akaja akaiona na kuridhika na wakakubaliana bei wakauziana na kupewa hati ya nyumba.

Na siku serikali wakaja sasa kuzivunja na wewe upo humo na waliwapa siku kadhaa muwe mmeshaondoka na wanajua wameshawalipa nyie na wewe upo humo unajua umenunua nyumba ya milele kwa hela ndefu kweli, hapo wakuu msaada utapata wapi? Ukashtaki sehemu ipi! Na Aliekuuzia alishatoweka labda yupo mkoa mwingine utampata wapi?

Hapo ndio utasema "nobody can stop raggae"
 
Mkuu, yaani wewe upo Sumbawanga halafu unaomba ushauri Jf??

Nijuavyo Mimi hapo Sumbawanga Kila nyumba ina mchawi hata mmoja.

Halafu Huo uwanja ulikua wa ajabu sana, yaani baiskeli na Bajaj zilikua zinakatisha katikati ya landing strip(only in Tz)
 
Mkuu, yaani wewe upo Sumbawanga halafu unaomba ushauri Jf??

Nijuavyo Mimi hapo Sumbawanga Kila nyumba ina mchawi hata mmoja.

Halafu Huo uwanja ulikua wa ajabu sana, yaani baiskeli na Bajaj zilikua zinakatisha katikati ya landing strip(only in Tz)
Hapana bajaji wala baiskeli zilizokuwa zinakatisha ata raia pia ni maalumu kwa ndege si unajua Viwanja vya ndege vya mikoani
 
Mtauziana vipi mali isiyohamishika tena yenye thamani kubwa namna hiyo pasipo kuwepo na ushahidi hata wa mjumbe wa nyumba kumi au mwenyekiti wa kijiji/mtaa?
Ok. Lakini ni mawazo tu ndugu
 
Huwezi kuwa na hati ya nyumba wakat umelipwa fidia ni ngumu, pili nyumba/ kiwanja huwezi kuuziana kama mitumba dukani

Ukitapeliwa ujue umelazimisha mwenyewe upigwe ili uwe fundisho duniani kwa wengine
 
ukitapeliwa hivyo unakuwa huna akili. mauzo ya viwanja yanafanyika officially Ofisi ya Ardhi Halmashauri na Commissioner wa Ardhi kanda. Hao wote wanajua matumizi ya maeneo hayo. Hiyo sio simu uuziwe kinyemela hata kama ana hati zipo taratibu zimewekwa kisheria
 

Similar Discussions

3 Reactions
Reply
Back
Top Bottom